24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Dk.Dau sasa Balozi Malaysia

Rais Dk. John Magufuli akimwapisha Dk. Ramadhani Dau kuwa balozi wa Tanzania nchini Malaysia Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Rais Dk. John Magufuli akimwapisha Dk. Ramadhani Dau kuwa balozi wa Tanzania nchini
Malaysia Ikulu jijini Dar es Salaam jana.

Na MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli amemwapisha   aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia.

Dk. Dau ambaye alilitumikia shirika hilo kwa miaka 19 tangu alipoteuliwa mwaka 1997 na Rais mstaafu Benjamin Mkapa na baadaye Jakaya Kikwete aliondolewa katika nafasi hiyo, Februari 15, mwaka huu.

Ingawa Rais Magufuli alimteua kuwa Balozi la-kini alikuwa hajampangia kituo cha kazi hadi jana alipoapishwa rasmi kuwa Balozi nchini Malaysia.

Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu, Gerson Msigwa alisema Dk. Dau aliapishwa   pamoja  na makatibu tawala wa mikoa mitatu.

Msigwa alisema Balozi Dau anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini humo, Dk. Aziz Ponary Mlima ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

“Rais Magufuli pia amewaapisha   makatibu tawala wa mikoa mitatu aliowateua mwishoni mwa wiki iliyopita.

Alitaja  walioapishwa kuwa  ni Eliya Ntandu anayekuwa Katibu Tawala wa kwanza wa Mkoa wa Songwe ulioanzishwa rasmi Februari, mwaka huu.

Wengine ni Adoh Mapunda ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Benedict ole Kuyan ambaye amestaafu.

“Tixon Nzunda ameap-ishwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Symthies Pangisa ambaye amestaafu,” alisema.

Msigwa alisema baada ya kuapishwa, Balozi Dau na makatibu tawala walikula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu, Salome Kaganda na kushuhudiwa na Rais Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles