30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

MSD, Sierra Leone kubadilishana uzoefu wa utendaji

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Bohari Kuu ya Dawa nchini(MSD) imekubaliana kushirikiana na Bohari ya Dawa ya Sierra Leone ikizamo kubadilishana taarifa za utendaji ili kuwasaidia bohari hiyo kuweza kukua na kufikia ukubwa wa MSD.

Akizungumza Aprili 29, 2024 baada ya mazungumzo na ugeni kutoka Sierra Leon uliokuja nchini kujifunza shughuli zinazofanywa na MSD, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai amesema kutokana na utendajikazi wa bohari hiyo umeendelea kuvutia wengi kuja kujifunza.

Amesema watawasaidia taasisi yao jinsi ya kuweza kushirikiana na wadau wengine ndani na nje ya Serikali ikiwemo kuunganisha mifumo yao na idara mbalimbali, kama watu wa fedha, utumishi, TEHAMA, wateja na wizara ya afya.

“Tunakumbuka Sierra Leon ni nchi ambayo ilikumbwa na matatizo ya amani ambayo yalivunja mfumo mzima wa afya, sasa wameamka na kujikung’uta na kuanza upya mfumo wao wa afya na sasa wamekuja huku kujifunza namna ya sisi tunavyofanya kazi zetu,” amesema Tukai.

Ameongeza kuwa moja ya kitu kilichowavutia zaidi ni ubunifu ambao MSD wamekuwa nao katika kufanya shughuli zao za kununua na kusambaza dawa lakini pia uhimilivu wa fedha na matumizi ya Tehama.

Kwa upande wake, Mfamasia Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Huduma za Dawa nchini, Daud Msasi amesema ujio wa wageni hao ni kuona wanaboresha bohari yao ya dawa inaboreshwa na kuimarika katika kutoa huduma.

Amesema nchi ipo tayari kuwapa ushirikiano wa kutosha kwa maslahi mapana ya wananchi wa Afrika.

“Ukiona mtu amechambua akaja akaswma akajifunze Tanzania inamaanisha tunafanya vizuri na ndio maana ndugu zetu hawa wakachagua kuja hapa kujifunza ni ugeni mzito ambao umeongozwa na Mganga mkuu wa nchi yao,” amesema Msasi.

Amesema viongozi hao wanauliza vitu vingi kwaajili ya kujifunza na wataendelea kuwapa ushirikiano na kujifunza na kuwa mfumo wa pamoja wa kununua dawa.

Naye, Mfamasia Mkuu na Mkurugenzi wa Huduma za Kifamansia Wizara ya Afya Sierra Leon, Dk. Moses Batema amesema wamefanya utafiti wa kutosha na kuona sehemu ya kwenda kujifunza ni Tanzania hivyo wameridhishwa na majadiliano walioyafanya lakini pia wamejifunza vitu vingi vitakavyowasaidia kuboresha bahari yao.

Amesema wametembelea MSD kwaajili ya kupata mafunzo mbalimbali ikiwemo kununua vifaa tiba na usambazaji wa dawa,ubunifu na mengine.

“Tilichagua MSD tunaamini tutapata kujifunza mambo mengi kutoka kwa MSD kupata ujuzi kutoka MSD na jinsi gani wanafanya kazi na wadau mbalimbali na nimefurahia mafunzo tuliyopata leo,”amesema Dk. Batema.

Naye Naibu Mkurugenzi wa Uendeshaji Wakala wa Taifa wa Usambazaji wa Dawa wa Sierra Leone, Jatu Abdulai amesema matumaini yake ni kuwa kati ya bohari za dawa hizo mbili wamebadilishana ujuzi katika masuala ya usambazaji wa dawa.

Amesema walipanga hilo kwaajili ya mafunzo na waliangalia katika Afrika MSD wamefanya vizuri katika kusambaza dawa hivyo wataendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles