30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Werema, Mkulo kutoa ushahidi kesi ya kina Kitillya

KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

ALIYEKUWA Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu  wa Serikali, Frederick  Werema na  Mbunge wa Kalenga, Godfrey  Mgimwa (CCM), wanatarajiwa kuwa miongoni mwa mashahidi 54 watakaotoa ushahidi katika kesi inayomkabili  aliyekuwa Kamishna  wa Mamlaka ya  Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitillya na wenzake wanne.

Hayo yalibainika jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati upande wa Jamhuri ukiwasomea washtakiwa mashtaka yao upya, idadi ya vielelezo na idadi ya mashahidi.

Akiwasomea washtakiwa Wakili wa Serikali Mkuu, Fredrick Manyanda, Tumaini Kweka wakisaidiana na George Barasa walidai katika kesi hiyo iliyohamia rasmi Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi itakuwa na mashahidi 54 wa upande wa Jamhuri, vielelezo 218 na maelezo ya washtakiwa wote watano.

Washtakiwa  hao wanakabiliwa na mashtaka 58 yakiwemo 49 ya kutakatisha fedha. Washtakiwa hao ni Kitilya, Kamishna wa Sera ya uchambuzi wa Madeni kutoka Wizara Fedha na Mipango, Bedason Shallanda, msaidizi wake Alfred Misana, maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon.


Wakili Barasa aliwataja mashahidi 54 wanaotarajia kuwaita kutoa ushahidi katika kesi hiyo kuwa miongoni mwao ni Mkulo, Werema, Mgimwa, Jane James, Omary Waziri, Ramadhani Kija.
Wakili Kweka alitaja vielelezo watakavyotoa mahakamani kuwa ni 218 ikiwemo hundi, vocha mbalimbali za malipo, magari na maelezo ya mahojiano ya washtakiwa wote.

Baada ya kumaliza mchakato huo Hakimu Shaidi aliwauliza washtakiwa kama wana kitu cha kuzungumza lakini washtakiwa wote walidai hawana cha kuongezea.

Hakimu Shaidi alisema baada ya hatua yote kumalizika mahakama inawahamishia washtakiwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kwa ajili ya kuendelea kusikiliza kesi yao.

Hadi kufikia hatua hiyo washtakiwa hao wameshakaa gerezani takribani miaka mitatu.

Katika hati ya mashtaka,  washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kughushi, moja la kuongoza uhalifu, 49 utakatishaji fedha, mawili ya kutoa nyaraka za uongo, kujipatia fedha kwa njia ya udanyanyifu moja na shtaka moja la kutoa nyaraka kwa nia ya kumdanganya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.

Wanadaiwa kuwa kati ya Machi 15, 2013 na Januari 10, 2014 ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa nia ya kudanyanya washtakiwa wote walijipatia Dola za Marekani milioni sita wakionesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji wa upatikanaji wa mkopo na zililipwa kupitia Kampuni ya Egma T Ltd.

Katika shtaka la utakatishaji fedha,  washtakiwa wote, Machi 18, 2013 na Januari 10, 2014 wakiwa jijini Dar es Salaam walitakatisha Dola za Marekani 6,000,000 kwa kuzitoa fedha hizo kupitia njia ya benki kwa jina la Enterprises Growth Market Advisors (EGMA) katika benki ya Stanbic Tanzania.

Pia katika kosa la kusababisha hasara kwa serikali, inadaiwa washtakiwa hao, Mei mosi mwaka 2012 na Juni mosi mwaka 2015 wakiwa jijini Dar es Salaam walijipatia Dola za Marekani milioni sita kama ada ya mkopo uliochukuliwa na Serikali ya Tanzania kutoka katika asilimia 1.4 hadi 2.4 na kusababisha serikali ipate hasara ya Dola za Marekani milioni sita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles