24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wanawake tusifanyiane ‘figisu’ – Dk. Chaula


NA VERONICA ROMWALD– DAR ES SALAAM

WANAWAKE wameshauriwa kuishi kwa upendo, umoja na mshikamano wa dhati kwani wana uwezo wa kutengeneza fursa nyingi zenye tija zinazoweza kuwasaidia kwenye maisha, familia na Taifa kwa ujumla.

Rai hiyo ilitolewa juzi jijini hapa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.  Zainab Chaula alipozungumza katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

“Katika maisha kila mmoja ana nafasi, ana mchango wake, mwanamke ana mchango mkubwa zaidi, sisi ni jeshi kubwa, tunao uwezo wa kufanya mambo makubwa na mazito na ili kuyafanya na kuyajenga lazima pawe na amani.

“Hivyo, wanawake lazima tuthamini kazi ya kila mtu, hakuna anayeweza kufanya jambo peke yake, tupendane, tushikamane tuwe wamoja, tusitengenezeane figisu (mizengwe),” alisema.

Aidha Chaula aliwapongeza wanawake na wafanyakazi wa JKCI kwa kazi nzuri wanayofanya ya kutibu wagonjwa wa moyo nchini huku akiweka wazi kwamba Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ameridhia kuipatia fedha kiasi cha Sh bilioni 1.5.

Awali, Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo JKCI, Delila Kimambo alisema katika kusherehekea siku hiyo waliwafanyia uchunguzi wa moyo wanawake 180 katika Soko la Kimataifa la Samaki Feri, Dar es Salaam.

“Takwimu za dunia zinaeleza asilimia 90 ya wanawake wana kiashiria hatari zaidi cha magonjwa ya moyo ikilinganishwa na wanaume ambao ni asilimia 10 tu, ndiyo maana tuliona vema kuwafanyia uchunguzi hasa kundi hili,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles