27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Vietnam yatangaza kumpokea Kim Jong Un

HANOI, VIETNAM

SERIKALI ya Vitenma kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imesema kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un atafanya ziara rasmi ya kwenda nchini humo katika siku za hivi karibuni.

Ziara hiyo inafanyika huku taifa hilo la Kusini-Mashariki mwa bara la Asia likiwa linajitayarisha kwa mkutano wa kilele kati ya Kim Jong Un na Rais wa Marekani, Donald Trump wiki ijayo ambao utafanyika katika mji wake mkuu wa Hanoi.

Taarifa ya wizara hiyo imeeleza kwamba Kim anaitembelea Vietnam kwa mwaliko wa Rais Nguyen Phu Trong ambaye pia ni katibu mkuu wa chama tawala cha Kikomunisti.

Mkutano huo wa kilele kati ya Kim na Trump utakaofanyika Febuari 27 hadi 28, unafuatia mkutano wao wa kihistoria wa mwezi Juni mwaka jana nchini Singapore.

Vyombo vya habari vya serikali Korea Kaskazini bado havikuthibitisha ziara ya Kim nchini Vietnam, wala kukutana kwake na Trump.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles