23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Samia ataka huduma bora za afya kwa wananchi

MWANDISHI WETU-ZANZIBAR

MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan. amewataka wanaotoa huduma katika sekta ya afya kutoa hduma bora.

Makamu wa Rais aliyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa jengo la kituo cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni ikiwa sehemu ya maadhimisho ya shamrashamra za kutimiza miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kutokana na hali hiyo aliwataka wataalamu wa afya nchini kutambua kuwa wanatakiwa kutumia utaalamu wao katika kuokoa maisha ya mama na mtoto ili kuepuka vifo vitokanavyo na uzazi kwa ajili ya kujenga Taifa lenye kizazi imara.

“Ni wajibu wenu kutumia utaalamu wenu na jukumu mlilopewa na Taifa katika kuleta mabadiliko ya kiutendaji na ufanisi katika sekta ya afya nchini,” alisema Samia

Jengo la Kituo cha Mama na Mtoto ni la ghorofa mbili na limegharimu jumla ya Sh bilioni 3.648 na kuzingatia watu wenye mahitaji maalumu.

Huduma zitakazopatikana kwenye jengo hilo la ghorofa mbili ni ya Mama na Mtoto, wodi ya wazazi na watoto, upasuaji kwa mama Wajawazito, vipimo X Ray, Utra Sound na maabara, ofisi za huduma za madaktari, wauguzi na wahudumu wengineo.

Mradi huo wa ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto ni utekelezaji kwa vitendo wa malengo halisi ya mwasisi wa Mapinduzi Matukufu za Zanzibar ya mwaka 1964 marehemu Mzee Abeid Amani Karume ambaye alidhamiria kuimarisha huduma ya Afya kwa wakulima.

Uzinduzi wa jengo hilo umerahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wakazi wa maeneo ya Kibweni, Mwanyanya, Bububu, Mbuzini, Mtoni, Kama, Mfenesini, Mahonda, Mtopepo na maeneo mengine.

Kwa upande mwingine Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Haji Omar Kheir, alisema serikali itaendelea kusimamia yale yanayopaswa kutekelezwa haswa kwenye huduma za Afya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles