30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ripoti: Rais Trump hana hatia

WASHINGTON, MAREKANI

RIPOTI yenye kurasa 448 kuhusu uchunguzi maalumu kubaini iwapo Serikali ya Urusi iliingilia Uchaguzi Mkuu wa urais nchini Marekani mwaka 2016 imewekwa wazi baada ya uchunguzi wa miaka miwili kumalizika nchini humo.

Uchunguzi huo uliongozwa na Robert Mueller, aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Upelelezi wa ndani wa Marekani, FBI na imebaini kuwa ni kweli Urusi ilijaribu kuingilia Uchaguzi huo. Hata hivyo, katika ripoti hiyo, haikubainika iwapo kampeni ya rais wa sasa, Donald Trump ilishirikiana na Urusi au raia yeyote wa Marekani.

“Baada ya uchunguzi wa miaka miwili, maelfu ya watu kujitokeza na mamia kutoa ushahidi, imebainika kuwa ni kweli Urusi ilijaribu kuingilia Uchaguzi wa Marekani, lakini wale waliomsaidia Rais Trump kufanya kampeni hawakuhusika,” amesema Mwanasheria Mkuu, William Barr.

Mawakili wa Trump wamesema kuwa ripoti hiyo ni ushindi mkubwa kwa upande wao, baada ya kushutumiwa hapo awali kuwa, Trump alisaidiwa na Urusi kuingia madarakani.

Pamoja na hilo, ripoti hiyo imeeleza kuwa Rais Trump alijaribu kushawishi kufutwa kazi kwa Mueller, aliyekuwa anaongoza uchunguzi huo. Trump amekuwa akisema kuwa hakuwahi kushirikiana na Urusi kushinda uchaguzi wa mwaka 2016.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles