30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Nanyamba aipigia debe Ruwasa

MWANDISHI WETU-DODOMA

MBUNGE wa Nanyamba, Abdallah Chikota (CCM), ameitaka Serikali ifanye maandalizi ya kutosha ili Wakala wa Maji Vijijini (Ruwasa) itakapoanza kazi, ifanye kazi kwa mafanikio.

Chikota aliyasema hayo bungeni jana alipokuwa akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa mwaka wa fedha 2019/20.

“Baada ya Bunge kupitisha mabadiliko ya sheria namba tano inayotoa nafasi ya kuanzishwa kwa Ruwasa, wakati umefika sasa kwa Serikali kufanya maandalizi ya kutosha ili mamlaka hiyo itakapoanza kutekeleza majukumu yake, ifanye kazi zake kwa ufanisi.

“Mamlaka ya Serikali za Mitaa zina hadhi tofauti, kwa hiyo, ili Ruwasa iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, kuna haja sasa kwa Serikali kuanza maandalizi ya kutosha ili mamlaka hiyo ikianza kazi, basi tusije tukailaumu kutokana na kukosa vitendea kazi.

“Pamoja na hayo, fedha zilizotengwa kwa ajili ya Wizara ya Maji ni vizuri zaidi zikitolewa zote kama zilivyopangwa ili miradi ya maji itekelezwe kama ilivyopangwa kwani njia hiyo itapunguza hoja za wabunge kujibu kwa wananchi wakati wa uchaguzi mkuu mwakani.

Akizungumzia jimbo lake, Chikota aliomba Wizara ya Maji itoe kibali cha utekelezaji wa mradi wa kutoa maji Mitema hadi Halmashauri ya Nanyamba, ili meneja anayetekeleza mradi wa Makonde, awe sehemu ya mradi huo.

“Kwa sasa, asilimia 45 ya wananchi wa Halmashauri ya Nanyamba, ndio wanaopata maji ila mradi huu ukitekelezwa, wananchi zaidi ya asilimia 85 watapata maji na hili ndilo jambo jema kwangu,” alisema Chikota.

Kwa upande wake, Mbunge wa Igalula, Mussa Ntimizi (CCM), alisema wabunge wengi wanataka maji yapatikane kwa urahisi majimboni kwao ili kuwaondolea kero wananchi.

Pamoja na hayo, Ntimizi alionyesha masikitiko yake baada ya jimbo lake kutojumuishwa katika maeneo yatakayopata maji kupitia mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles