Na Brighiter Masaki
Mkuu waMkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametangaza msakokwa wafanyabiashara wadogo wasiokuwa na vitambulisho vya ujasiliamali vilivyo anza kutolewa mapema mwanzoni mwa mwaka huu.
Msako huo ni moja ya mkakati wa ukusanyaji mapato kupitia wafanyabiashara hao.
Paul Makonda amesema June3 mwaka huu ni marufuku kwa mfanyabiasharayoyote mdogo kujishughulisha na biashara ndani ya mkoa huo bila kuwa na kitambulisho maalumu cha utambuzi kilichotolewa na Rais Dk John Magufuli.
Sambamba na hilo,mkuu wa mkoa huyo amewasihi wafanyabiashara hao walipe kodi ili waongeze wastani wa pato la taifa kupitia kodi.
Aidha Makonda amewataka wafanyabiashara wasiopata vitambulisho lakini wanavigezo vya kuvipata wafike sehemu husika ikiwemo ofisi za wakuu wa mikoa ili kuvipata.
Amesema takwimu kubwa zinaonyesha kuwa idadi ya wafanyabiashara wasiokuwa na vitambulisho ni kubwa.