27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa awahakikishia wananchi maboresho sekta ya afya

MWANDISHI WETU-MWANZA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa  amefungua mradi wa ujenzi na ukarabati wa kituo cha afya cha Kata ya Koromije wilayani Misungwi na amewahakikishia wananchi kuwa Serikali imejipanga kuboresha huduma za afya.

Alisema uboreshaji huo unahusisha ujenzi wa chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kujifungulia, wodi ya mama na mtoto na wodi ya wanawake na wanaume   na chumba cha kuhifadhia maiti. Uboreshaji huo unagharimu Sh milioni 500.

 “Hapa zamani kulikuwa na zahanati yenye jengo moja, tumeamua kuboresha na kupandisha hadhi na kuwa kituo cha afya. Rais Dk. John Magufuli anataka wananchi wapatiwe huduma muhimu zikiwamo za afya karibu na makazi yao”.

Alisema pia kuwa hakuna kijiji chochote nchini kitakachoachwa bila ya kuunganishiwa umeme katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA), vikiwamo na vya wilaya ya Misungwi tena kwa gharama nafuu.

 “Rais wetu, Dk. John Magufuli anajali sana wananchi wake, hivyo ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na wilaya yenu hii ya Misungwi. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.”

 Waziri Mkuu aliongeza  lengo la Serikali ni kufikisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzania na vile ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi ya taifa vitafungiwa sola, jambo ambalo litafungua fursa za ajira na kukuza uchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles