24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Jeshi la Sudan lakataa kukabidhi madaraka


KHARTOUM, SUDAN

JESHI nchini Sudan ambalo linashikilia madaraka tangu Aprili 11, mwaka huu baada ya kumng’oa Rais Omar al-Bashir, aliyekuwa ameongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 30, limekataa matakwa ya wananchi wa nchi hiyo ambao wamekuwa wakiandamana na kupinga mpango wake wa kuwa madarakani kwa kipindi cha mpito cha miaka miwili kabla ya kuitishwa uchaguzi na kukabidhiwa Serikali ya kiraia.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, limemkariri Luteni Jenerali Salah Abdelkhalek kuwa Baraza la Jeshi nchini Sudan halitaruhusu raia yeyote kuchukua nafasi za juu katika Baraza la Uongozi nchini humo wakati wa Serikali ya mpito. Luteni Jenerali Abdelkhalek, amesema labda wanaweza kuzingatia kuwapa nafasi sawa za ujumbe katika baraza hilo.

Wakati Luteni Jenerali Abdelkhalek, akisema hayo, waandamanaji wanaendelea kuandamana kwa kukaa kwa wingi nje ya ofisi kuu ya jeshi la nchini hiyo wakilitaka kuachia madaraka.

Viongozi wa waandamanaji wamelishutumu jeshi kukataa kufanya majadiliano kwa nia njema na kuhamasisha masilahi ya Bashir. Viongozi wa Jeshi wanasema kuwa wanahitajika kuchukua hatua zinazohitajika ili kuhakikisha kuwa wanaongoza na usalama wa taifa hilo.

Wajumbe saba wa baraza ambalo linaongozwa na Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, ambaye aliiambia BBC mwezi uliopita kuwa yuko tayari kukabidhi madaraka kama watafikia makubaliano na viongozi wa uraia.

Viongozi wa upinzani walisema juzi kuwa mapendekezo ya nakala ya katiba kwa Baraza la Jeshi kueleza mapendekezo waliokuwa nayo katika kipindi hiki cha uongozi wa mpito. Wanasema kwa sasa wanasubiri majibu. Nakala ya mapendekezo na majukumu ya baraza jipya haijaainisha nani atakuwepo katika baraza.

Umoja wa Afrika ulikabidhi utawala kwa viongozi wa jeshi kuwa Aprili 15, mwaka huu iwe mwisho wa Jeshi hilo kuongoza Sudan, lakini hadi sasa wana siku 60 madarakani au kukutana na baraza la uongozi.

Kiongozi wa zamani wa Sudan, Bashir mwenye umri wa miaka 75, amehamishiwa katika gereza la Kobar lililopo mji mkuu wa Khartoum, baada ya siku kadhaa tangu amekamatwa. Mwendesha mashtaka ametaka rais wa zamani kuhojiwa kwa makosa ya utakatishaji fedha na kufadhili ugaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles