26.2 C
Dar es Salaam
Friday, December 3, 2021

Zambi aishukuru TFF kupeleka fainali ya FACup Lindi


Hadija Omary, Lindi

Halmashauri ya Manispaa ya Lindi imetakiwa kuboresha Uwanja wa michezo wa Ilulu kwa ajili ya kufanikisha mashindano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) baada ya mkoa huo kupewa heshima ya kuwa mwenyeji wa fainali za mashindano hayo itakayopigwa Mei mwaka huu.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Godfrey Zambi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake ambapo amewataka kwa pamoja wajipange  vema kufanikisha fainali hiyo inafanyika kwa mafanikio ili ilete hamasa kwa wageni watakaokuja na kutumia uwanja huo.

Hata hivyo Zambi ametumia fursa hiyo kulipongeza Shirikisho la Soka nchini, kwa kuchagua mkoa huo kuandaa fainali hizo kubwa pamoja na kutoa msaada wa matengenezo ya uwanja wa kuchezea.

Mkoa wa lindi kwa mwaka huu unatarajia kuwa mwenyeji wa fainali hizo, Tamasha la vijana pamoja na kilele cha mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa matukio ambayo yanatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Ilulu ulio manispaa ya lindi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,875FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles