25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Yanga sasa kuchaguana Machi 10

ZAITUNI KIBWANA-DAR ES SALAAM

UCHAGUZI Mkuu wa klabu ya Yanga, uliosimamishwa kutokana na baadhi ya wanachama kufungua kesi mahakamani,  sasa umepangwa kufanyika Machi 10, mwaka huu.

Awali, uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Januari 13, mwaka huu, lakini uliahirishwa baada ya baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kuweka pingamizi mahakamani.

Habari za ndani ambazo gazeti hili ilizipata, zilisema viongozi wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wenzao wa kamati ya uchaguzi ya klabu ya Yanga, wamekubaliana kwa pamoja kufanyika uchaguzi huo.

“Tumekubaliana kwa pamoja yaani kamati ya TFF na ile ya Yanga, tumeondoa tofauti zetu hivyo sasa uchaguzi huu utafanyika Machi 10 mwaka huu,” alisema.

Wakati chanzo hicho kikisema hayo, MTANZANIA lilimtafuta Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Ally Mchungahela, ambaye aligoma kuweka wazi lakini akasema leo watakutana na kamati mpya ya Yanga kujadili kwa pamoja hatima ya uchaguzi huo.

“Nipo njiani nakuja Dar es Salaam kwa ajili ya mkutano wa pamoja na viongozi wa Yanga tutakaokutana kesho ( leo) hivyo baada ya hapo ndipo itajulikana nini tumekiamua,” alisema.

Awali, uongozi wa Yanga uliunda kamati mpya ya uchaguzi mdogo ikiongozwa na wabunge wanne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kamati hiyo mwenyekiti wake ni Venance Mwamoto ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Katibu wake ni  Mbunge wa Jimbo la Manonga mkoani Tabora, Seif Gulamali, Dunstan Kitandula ambaye ni Mbunge wa Mkinga na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Saidi Mtanda.

Uchaguzi huo ni wa kujaza nafasi zilizoachwa wazi ikiwemo nafasi ya Mwenyekiti, Yussuph Manji, aliyejiuzulu umekuwa ukipigwa danadana kutokana na kuingia mkanganyiko kuhusu nafasi ya Manji igombewe au isigombewe.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,277FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles