29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wapinzani wataka wakandarasi wazawa walipwe

ARODIA PETER-DODOMA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeishauri Serikali kutafuta fedha za kulipa wakandarasi wazawa ambazo hazikutolewa katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2018/2019 iliyoidhinishwa na Bunge.

Akiwasilisha maoni hayo bungeni juzi, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Moshi Kakoso, alisema pamoja na ongezeko la fedha za miradi ya maendeleo kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutoka Sh trilioni 4.2 kwa mwaka 2018/ 2019 hadi Sh trilioni 4.8 kwa mwaka wa fedha ujao wa 2019/2020, lakini kwa upande wa fedha za miradi ya maendeleo kwa sekta ya mawasiliano, hakuna fedha yoyote iliyotengwa.

“Hata hivyo, kamati ilielezwa kuwa fedha hizo zitatolewa kutoka katika fedha za mkongo wa taifa wa mawasiliano.

“Kamati inasisitiza kuwa ni muhimu fedha hizo zitolewe ili kuendeleza miradi muhimu iliyokuwa inaendelea, kama vile mradi wa anuani za makazi na misimbo ya posta, mkongo wa taifa wa mawasiliano na ujenzi wa kituo cha kutengeneza vifaa vya Tehama,” alisema.

Kuhusu bandari, kamati hiyo ilishauri Serikali kubakisha angalau asilimia 40 ya makusanyo ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), ili yaendeleze baadhi ya miradi katika bandari zake.

“Pamoja na upanuzi na ukarabati wa Bandari ya Dar es Salaam unaoendelea, kamati inasisitiza ili kuongeza ufanisi na mapato katika bandari hiyo, juhudi za makusudi zifanyike kuhamisha Gati la Mafuta la Kurasini (KOJ) na kujenga gati namba 13 na 14,” alisema.

Pia walilalamikia Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kulundikiwa miradi mingi tofauti na uwezo wake.

Katika hotuba yao iliyosomwa na Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga kwa niaba ya Waziri Kivuli wa wizara hiyo, James Mbatia, alisema hivi karibuni kumejitokeza malalamiko mengi kutoka kwa Serikali ikilalamikia utendaji usioridhisha wa TBA.

“Moja ya malalamiko hayo ni pamoja na kutumia gharama kubwa zisizoridhisha katika baadhi ya miradi zisizolingana na thamani ya majengo husika pamoja na kuchelewa kukamilisha miradi husika.

“Tunaona tatizo hilo linatokana na ukweli kwamba TBA wanapewa kwa kulazimishwa kazi za Serikali bila wao kuingia kwenye mfumo rasmi wa ununuzi huku uwezo wao wa kufanya kazi ukiwa ni mdogo.

“Tunapenda kufahamu hiyo miradi inayotolewa na wizara, taasisi za Serikali na kuletwa tu TBA kama zawadi au kuna utaratibu wa kufuata sheria ya ununuzi unafanyika na kama utaratibu huo haufanyiki ni hatua gani za kinidhamu kwa wahusika zinachukuliwa.

“Pia taarifa inaonesha kuwa TBA inahudumia miradi 90 ya design & build kwa nchi nzima, hii ni miradi mingi sana na kwa kawaida si rahisi thamani ya fedha ikaonekana kwa taasisi moja kama hiyo,” alisema Kiwanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles