27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wagonjwa nane wapandikizwa figo Benjamin Mkapa


Arodia Peter, Dodoma

Hospitali  ya Benjamini Mkapa iliyopo jijini Dodoma,  imefanikiwa  kupandikiza figo kwa wagonjwa nane kwa kipindi cha miaka miwili tangu kuanzishwa kwake.

Hayo yalisemwa na daktari bingwa wa figo hospitalini hapo Dk. Kessy Shija, jana Mei 4,  alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliokuwa kwenye ziara ya kutembelea miradi  inayofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani humo.

Dk. Shija alisema kuanzishwa kwa huduma hiyo ya kibingwa hospitalini hapo kumepunguza gharama kwa wagonjwa kwenda kupata matibabu hayo nje ya nchi, hususani India.

“Niwashauri Watanzania kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kwa sababu  magonjwa ya kudumu kama figo yanachukua wastani wa Sh, 200,000 hadi 250,000 kwa wiki ambazo ni gharama za kusafishwa, ambapo  kwa matibabu ya kupandikizwa figo huchukua wastani wa hadi Sh, 6, 000, 000 kwa mgonjwa mmoja,” alisema.

Aidha Dk. Shija alisema mbali na figo, hospitali hiyo pia inatoa matibabu ya kibingwa kwa wagonjwa wa moyo kama ilivyo kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles