24.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

UN yataka uchaguzi huru na wa haki

KINSHASA, DRC

KATIBU mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inahakikisha nchi hiyo inafanya uchaguzi huru na wa haki pamoja na wananchi wote kupatiwa fursa sawa za kushiriki zoezi hilo linalotarajiwa kufanyika leo nchini humo.

Guterres amesema hayo juzi wakati akitoa ujumbe wake kwa DRC, huku wananchi waliotimiza masharti ya kupiga kura wakitazamiwa kuelekea katika masanduku ya kupigia kura kumchangua kiongozi atakayerithi mikoba ya Rais Joseph Kabila.

Wito wa Katibu Mkuu wa Umoja huo usisitiza kuwa pande zote husika za kisiasa kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanyika kwa uhuru na amani.

“Vyombo vya dola, viongozi wa kisiasa, maafisa wa uchaguzi na asasi za kiraia zinapaswa kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na mazingira ya kufanyika uchaguzi huru na wa haki, na kwa amani.”

Guterres amewataka Wakongamani kutumia fursa hiyo ya uchaguzi aliyoitaja kuwa ya kihistoria, kuzipa nguvu taasisi za kidemokrasia nchini humo.

Tayari taasisi muhimu za ndani na nje ya nchi zimeelezea wasiwasi wao kuhusu uwezekano wa kutokea machafuko wakati na baada ya zoezi hilo.

Hata hivyo taarifa ya Umoja wa Mataifa imewataka wadau wote kutekeleza wajibu wao na kujiepusha na kauli au vitendo vinavyoweza kuchochea ghasia ili kuhakikisha kuwa zoezi hilo la kidemokrasia linafanyika kwa amani.

Mbali na kuhitimisha uongozi wa Kabila ambaye yuko madarakani toka mwaka 2001, wapiga kura pia watawachagua wabunge na wawakilishi wa mabunge ya mikoa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles