26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Uhakiki mali CCM wawakimbiza wawekezaji wenye mikataba feki

BENJAMIN MASESE

Wawekezaji 48 kati ya 160 waliokuwa  wanafanyia shughuli zao za  uchumi kwenye majengo ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM)  Wilaya za Nyamagana na Ilemela   Mwanza wametimuliwa.

Habari zinasema  wengine wamejisalimisha    baada ya chama hicho  kufanya  uhakiki na kuwabaini  baadhi yao walipata vyumba hivyo kwa njia zisizo halali.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli alikuwa akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kuhitimisha   uhakiki huo.

Alisema  walibaini baadhi ya wawekezaji  hawakuwa na mikataba halali kutoka kwa uongozi wa chama hicho, hivyo ilibidi waondolewe.

Kalli alisema  baadhi ya wawekezaji walikuwa wamepangishwa na watu ambao wana mikataba halali  kutoka kwenye uongozi wa CCM jambo ambalo ni kinyume na  kanuni za fedha na mali za chama na jumuiya kama inavyoelekeza katika toleo la 2018.

“Kama mnakumbuka Mwenyekiti wetu, Rais Dk. John Magufuli alisema ni lazima mali za  CCM  zijulikane, tujue thamani yake, tuwatambue wawekezaji wetu katika majengo yetu na mambo mengine, ndiyo maana kama mkoa hatua hiyo imeanza na tumebaini mambo mengi.

“Mfano katika jengo la CCM la mkoa  yaani hapa tulipo kuna ghorofa tano na tunao wawekezaji wengi.

“Lakini baada ya kufanya uhakiki  wapo ambao baadhi  tumewakuta hawana sifa   za kuendelea kubaki, tumewaondoa na wengine wamejisalimisha tufakanya mazungumzo na wamebaki ambako  vyumba vinne vipo wazi likiwamo eneo la duka la jumla  kwa matumizi ya benki.

“Katika kitenga uchumi chetu pale Uwanja wa CCM Kirumba baada ya kuhakiki kila chumba tumebaini zaidi ya vyumba 43 vilikuwa na mikataba inayovunja  kanuni za fedha na mali za chama.

“Hivyo tumewaondoa na vipo wazi kwa watu wengine watakaofuata taratibu, hatukubaliana kuona chama kikiwa na vitenga uchumi vyake kisha wanufaike wachache,”alisema.

Kalli alisema  wakati akikabidhiwa ofisi mwezi mmoja uliopita  na mtangulizi wake katika nafasi ya ukatibu,  Adam Ngallawa, CCM ilikuwa ikiwadai wawekezaji hao zaidi ya  Sh milioni 133.

Alisema alilazimika kuitisha kikao cha mazungumzo  ya urafiki na kuwapa elimu jambo lililoongeza kasi ya ulipaji.

Alisema ndani ya mwezi mmoja zimeweza kukusanywa  Sh milioni 60 ambazo ni sehemu ya Sh milioni 133 ya  madeni ya wawekezaji .

Kalli alisema  imani yake ni kuhakikisha ndani ya miezi minne atakuwa amafanikiwa kukukusanya kiasi kilichobaki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles