27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Sumaye augua ghafla Tanga, akimbizwa Muhimbili

AGATHA CHARLES, DAR

WAZIRI Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Frederick Sumaye, ameugua ghafla akiwa jijini Tanga alikokuwa akifanya ziara ya chama hicho.

Taarifa iliyotolewa jana mchana na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari wa chama hicho, Tumaini Makene, ilisema Sumaye alipopatwa na shida hiyo alipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga.

Hata hivyo, Makene alisema Sumaye alitarajiwa kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa uchunguzi zaidi.

“Baada ya kutibiwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga hali yake inaendelea vizuri, amepumzika wakati mipango ya kumsafirisha kwenda Muhimbili leo (jana) kwa uchunguzi zaidi inafanyika,” alisema Makene.

Baadaye jioni, Makene alisema Sumaye alifikishwa Muhimbili na kupokelewa kitengo cha dharura.

MTANZANIA Jumamosi lilimtafuta Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, John Steven, alisema anafuatilia taarifa hiyo na atawasiliana na mwandishi wa habari hii.

“Ngoja nifuatilie nijue, nikikuta hakuna foleni ya wagonjwa nitakujulisha mapema zaidi. Nitakupigia mwenyewe,” alisema.

Baadaye, Steven, alipiga simu na kueleza kuwa ni kweli Sumaye alipokelewa hospitalini hapo saa 10:30 jioni.

“Ni kweli amepokelewa na anapatiwa huduma za awali ikiwamo vipimo,” alisema Steven.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,451FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles