28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 12, 2024

Contact us: [email protected]

Standard Chartered yaja na mapinduzi ya dijitali

MWANDISHI WETU-DAR E SALAAM

BENKI ya Standard Chartered Tanzania, jana ilizindua mfumo mpya wa matumizi ya teknolojia ya kidijitali ambayo inawezesha wateja wake kupata huduma zaidi ya 70 kwa urahisi zaidi.

Mfumo huo unawezesha wateja wa benki hiyo kujipatia huduma za kibenki kulingana na matakwa yao, ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga kwa kupakua programu hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani, alisema programu hiyo inarahisisha zaidi upatikanaji wa huduma za kibenki hapa nchini, ikiwa ni mwendelezo wa safari yao muhimu ya matumizi ya teknolojia za kidijitali.

“Huduma hii inadhihirisha dhamira yetu ya kuendeleza kuwekeza katika kuleta mapinduzi ya teknolojia za kisasa, kujenga mifumo na kuimarisha watu wetu kwa ujuzi wa ngazi ya kimataifa na kuleta mabadiliko ya uhakika ya matumizi ya teknolojia ya kidijitali nchini Tanzania.

“Matumizi ya teknolojia za kisasa za kidijitali kwetu kuna maana ya kuleta mapinduzi kutoka mifumo ya utoaji wa huduma za kibenki ya zamani kwa lengo la kuboresha huduma kwa wateja wetu kuendana na mabadiliko yaliyopo kwa wakati huu,” alisema Rughani.

Naye Mkuu wa huduma za kibenki wa Standard Chartered, Ajmair Riaz, alisema wateja wa zama za sasa wanahitaji washirika ambao wanaweza kuwapatia huduma zinazopatikana kwa urahisi na gharama nafuu.

“Programu yetu hii mpya imebuniwa kuleta suluhisho kwa matakwa ya wateja wetu baada ya kufanyia kazi maoni kuhusu nini wanahitaji, mfumo huu utawezesha kupata huduma zote za kibenki kupitia simu ya mkononi kwa urahisi.

“Kwa mara ya kwanza katika safari yetu hii ya kuleta mapinduzi ya teknolojia ya kidigitali katika upatikanaji wa huduma za benki, mteja anaweza kufungua akaunti ndani ya muda wa dakika 15 tu,” alisema mkuu huyo wa huduma wa benki hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles