24.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Simba Queens yaipania Tanzanite leo

Na GLORY MLAY- DAR ES SALAAM

KOCHA wa Simba Queens, Antony Makunja, amesema wamejipanga kuibuka na ushindi dhidi ya timu ya Tanzanite katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara (WPL), utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Makunja, alisema timu yake imefanya maandalizi mazuri na wanaamini watakuwa wa kwanza kuchukua pointi tatu wakiwa ugenini.

Alisema malengo yao ni kuanza vizuri msimu unaokuja wa ligi hiyo ili waweze kutwaa ubingwa unaoshikiliwa na JKT Queens.

“Tupo vizuri wachezaji wana ari ya kucheza ligi kuu, hivyo tunawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kwa lengo la kuhamasisha ushindi,” alisema Makunja.

Msimu uliopita, Simba Queens ilishika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi nne sawa na Evergreen zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,400FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles