24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Simba kuwasha moto kwa AS Vita

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, timu ya Simba, leo wanatarajia kumenyana na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kwenye mchezo wa hatua ya makundi jijini Kinshasa.

Simba wataivaa AS Vita ikiwa na kumbukumbu ya kuinyuka JS Saoura ya Algeria mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Timu hiyo imepangwa Kundi D pamoja na Al Ahly ya Misri, AS Vita ya DRC na JS Saoura ya Algeria.

Mabingwa hao watetezi wa Tanzania, wanaongoza kundi hilo wakiwa na pointi tatu, sawa na Al Ahly iliyo nafasi ya pili kutokana na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa, AS Vita ikiwa katika nafasi ya tatu na JS Saoura ikikamata mkia, zote  zikiwa hazina pointi.

Simba waitavaa AS Vita wakimkosa  mshambuliaji wake, John Bocco,  Erasto Nyoni na Shomari Kapombe, ambao ni majeruhi.

Timu hiyo inahitaji kuendeleza ushindi kutokana na kuwa na rekodi nzuri ya matokeo katika mechi zao za nyuma.

Simba ilitinga hatua ya makundi baada ya kuitoa mashindanoni Nkana FC ya Zambia kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-3, ikianza kuchapwa mabao 2-1 mjini Kitwe, kabla ya kushinda mabao 3-1 nyumbani katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussems, aliweka wazi kuwa mipango yake ni kucheza soka la kushambulia na kupata pointi tatu muhimu ugenini na si kwenda kukaba pekee.

“Nafahamu mchezo utakuwa ni mgumu kutokana na uwezo wa wapinzani wetu ambao tutaenda kukutana nao, lakini hata hivyo nimekiandaa kikosi changu kwa ajili ya kushambulia na kupata ushindi,” alisema.

Alisema mara nyingi mechi za ugenini zinakuwa na ushindani na hasa aina ya timu ambayo wanaenda kucheza nayo,  ila ushindi waliopata kwenye mechi zilizopita zimewapa morali kubwa ya kuendeleza ubabe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles