24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Sidiria inayoweza kugundua saratani ya matiti

JULIANA Rios Cantu mwenye umri wa miaka 18 raia wa nchini Mexico, amevumbua sidiria inayoweza kugundua saratani ya matiti.

Kwa mujibu wa mtandao wa BBC, Juliana ametengeneza sidiria hiyo akisema itatoa dalili kwa mtu mwenye ugonjwa huo.

Sidiria hiyo iliyopewa jina la Eva, aliitengeneza na marafiki zake watatu na kuanzisha kampuni hiyo kwa pamoja.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa sidiria hiyo inaweza kupima viwango vya joto, kuviweka katika programu na kumwelezea mhusika kuhusu mabadiliko yanayomsumbua.

Wanawake wanaohitaji sidiria hiyo watalazimika kuivaa kwa dakika 60 hadi 90 kwa wiki ili kupata vipimo vya sawa.

Tayari sidiria hiyo imefanyiwa majaribio na itafanyiwa vipimo vingine vya kimatibabu kabla ya wataalamu wa ugonjwa wa saratani kuipendekeza kuwa njia ya kugundua saratani.

Anna Perman kutoka kituo cha utafiti cha Uingereza kiliiambia BBC kwamba “Tunajua kwamba uvimbe huo una mishipa isiyo ya kawaida ya kupitisha damu na tunajua kwamba kasi ya damu katika mishipa sio thibitisho kuwa mtu anakabliwa na saratani”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles