29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

Serengeti Boys kuikabili Austraria

JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM

TIMU ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys, leo itashuka dimbani kuvaana na Austraria katika michuano ya maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana (Afcon), nchini Uturuki.

Michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na lile la Ulaya (UEFA), imelenga kuzipa majaribio timu zitakazoshiriki michuano hiyo ya Afcon.

Katika mchezo uliochezwa juzi katika Uwanja wa Emirhan Sports Complex, Antalya nchini Uturuki, Serengeti Boys iliambulia kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Guinea.

Serengeti Boys iliyopo kundi A, mara baada ya kumalizana na Austraria watakabiliana na wenyeji wa michuano hiyo, Uturuki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles