27.8 C
Dar es Salaam
Monday, December 6, 2021

Samia aeleza ugumu kuondolewa VAT umeme Z’bar

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesema  haikuwa kazi rahisi katika hoja ya kuondoa Kodi ya Ongezeko la thamani (VAT) kwa umeme unaouzwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwenda Shirika la Umeme la Zanzibar (Zeco).

Hivi karibuni, Baraza  la Mawaziri liliridhia kufuta  VAT kwa umeme unaouzwa na Tanesco kwa  Zeco na kufuta malimbikizo ya deni la kodi hiyo lililokuwa limefika Sh bilioni 22.9.

Alikuwa akizungumza juzi wakati akifungua kikao kazi cha mawaziri na manaibu mawaziri wa  Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.  Kikao hicho pia kilihudhuriwa na  makatibu wakuu wa pande zote mbili. 

Makamu wa Rais alisema   Baraza la Mawaziri la Muungano na Zanzibar limekutana kwa miaka kadhaa kujadili suala la umeme wa Zanzibar  lakini ufumbuzi wake haukuweza kupatikana.

“Kwa mfano suala la umeme ufumbuzi wake ambao ulipatikana juzi, imefanyika kazi ndiyo ufumbuzi umepatikana lakini huko nyuma tuliishakutana miaka na miaka lakini hakuna   ufumbuzi.

“Nasema hivi kuonyesha kwamba kikao hichi kina mambo mchanganyiko, si sheria na katiba tu zinazofanya kazi, kuna mengine ‘concidaration’ nyingine inabidi ziingie,” alisema alisema Samia.

Alisema kikao hicho hujadili mambo mengi kwa urafiki huku kinachobaki huwa ni utekelezaji.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amemkabidhi hati ya kiwanja Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, chenye ukubwa wa  ekari 30 kwa ajili ya kujenga ofisi mbalimbali za serikali hiyo   Dodoma.

Akizungumza wakati akikabidhi hati hiyo, Makamu wa Rais  alisema hati hiyo inatolewa ikiwa ni ukaribisho wa kuhamia Dodoma.

“Sisi tumeshahamia Dodoma, wizara zote, mawaziri, makatibu wakuu wapo Dodoma,ujenzi wa wizara unaendelea katika mji wa serikali Ihumwa na nadhani mwishoni mwa mwezi huu wizara zitahamia huko,” alisema Samia.

Awali,   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema ukubwa wa kiwanja hicho ni sawa na viwanja 10 vilivyotolewa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za wizara za Jamhuri.

“Utoaji wa kiwanja hiki ni utekelezaji wa maelekezo aliyotatoa Rais Dk. John Magufuli la kutayarisha eneo, kulipanga na kulipima kwa ajili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na tulishatoa pia kwa mabalozi wa nchi mbalimbali pia,” alisema Lukuvi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,340FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles