23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Ruto aipasua kichwa upinzani

ISIJI DOMINIC

HAMNA ubishi mawazo ya wanasiasa wengi nchini Kenya, yameelekezwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 ikiwa bado zimebaki takribani miaka mitatu Rais Uhuru Kenyatta amalize muda wake.

Siasa hizi za mwaka 2022 zinaonekana kumkera Rais Uhuru ambaye mara kadhaa katika hotuba zake amezikemea akiwataka wanasiasa hususan waliochaguliwa kuwatumikia wananchi.

Aidha Rais Uhuru anaghadhabishwa na wanasiasa kutumia majukwaa ya kisiasa au hata kwenye mazishi kuwapiga vita wateule wanaoongoza taasisi mbalimbali zinazopambana na ufisadi.

Dhamira ya Rais Uhuru alipochaguliwa kuhudumu muhula wake wa pili ni kupambana na ufisadi akiwateua makachero kuongoza taasisi za Serikali hususan Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ofisi ya Mkurungezi wa Mashitaka ya Umma (DPP) na Tume ya Kupambana na Ufisadi (EACC).    

Wanasiasa wamegeuza vita dhidi ya ufisadi vina dhamira ya kuwalenga baadhi yao ili wasigombee uchaguzi mkuu ujao. Ofisi za DCI, DPP na EACC kwa miezi kadhaa sasa zimeonekana kutokutishiwa na wanasiasa na wamethubutu kuwafikisha mahakamani lakini kinachowakera Wakenya ni dhamana ndogo inayotolea na majaji ambao hata hivyo wamesisitiza wanaongozwa na sheria na lazima ushahidi uwe na nguvu.

Katika mapambano dhidi ya ufisadi, baadhi ya wanasiasa kutoka chama tawala cha Jubilee, wamekuwa wakilalamika yanamlenga Naibu Rais William Ruto ambaye ameweka wazi nia yake ya kuwania urais mwaka 2022.

Mapatano kati ya Rais Uhuru na kinara wa upinzani, Raila Odinga, ambayo yameleta utulivu nchini Kenya, yanawaweka njia panda wafuasi wa Ruto ambao wanadai Naibu Rais amekuwa akiachwa nyuma kwenye maamuzi mengi.

Wanasiasa wa upinzani nao wanamuunga mkono Rais Uhuru kwa hatua anazozichukua hususan vita dhidi ya ufisadi huku wakimshutumu Ruto kushindwa kutekeleza kwa ufanisi ajenda nne kuu na badala yake kumshambulia kwa maneno Raila.  

Ni katika azma hii ya kupambana na Naibu Rais wengi wakitafsiri ina lengo la kumdhoofisha kisiasa, tumeshuhudia hivi karibuni Seneta wa Kaunti ya Siaya, James Orengo, akiweka nia yake ya kupeleka hoja bungeni ya kutokuwa na imani na Ruto.  

Hoja hiyo imeungwa mkono na Katibu Mkuu wa ODM, Edwin Sifuna, akisisitiza Ruto ni kikwazo katika vita dhidi ya ufisadi.  

Alisema ODM inaunga mkono hoja ya kutokuwa na imani na Ruto akitolea mifano ya matamshi yake ya nyuma pamoja na washirika wake dhidi ya Mkurugenzi wa DPP, Noordin Haji na DCI George Kinoti wasiwashitaki watuhumiwa wa uhujumu uchumi. 

“Kama kura ya kutokuwa na imani itamwondoa (Naibu Rais), basi bora iwe hivyo,”alisema Sifuna. 

Hata hivyo, wanasiasa wanaomuunga mkono Ruto wamesema wanaisubiri hiyo hoja kwa hamu bungeni na kusisitiza hawataipitisha kwa sababu hiyo hoja ni ya Raila na Orengo ambaye ni mwandani wa kinara huyo wa upinzani anatumika. 

Kura ya kutokuwa na imani na Ruto ni mtihani si tu kwa wabunge lakini kupata tafsiri sahihi ya sheria ni namna gani Naibu Rais ambaye kuchaguliwa pamoja na Rais anaweza kuondolewa madarakani.  

Mchambuzi wa siasa nchini Kenya ambaye pia ni wakili maarufu, Ambrose Weda, alisema hatua hiyo itakuwa ngumu ukizingatia Naibu Rais hana mashitaka yanayohusu makosa ya jinai na pia kura hiyo itamshtua Rais Uhuru kwa sababu akiruhusu naibu wake kuondolea kwa staili hiyo hata yeye yanaweza yakamfika siku za usoni.  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,695FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles