25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RC Hapi akwepa mtego wa Waziri Mkuu

MWANDISHI WETU-DODOMA

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amejikuta akipona baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kuagiza kampuni zote zinazosambaza nguzo za umeme kuzitaka zilipe ushuru wa halmashauri wanakotoa nguzo hizo wa asilimia tano ya gharama ya kila nguzo kama ilivyoelekezwa na Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa.

Agizo hilo amelitoa jana mjini hapa katika kikao alichokiitisha kwa kumtaka Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi, wenyeviti wa halmashauri pamoja na Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani kwenda mjini Dodoma na watoe maelezo kwa nini wamezuia nguzo za umeme hali ya kuwa wananchi wanataka huduma hiyo.

Akitoa agizo hilo baada ya kupata taarifa kuhusu kampuni ya New Forest ambayo inamkataba na TANESCO wa kusambaza nguzo za umeme, kwa muda mrefu kampuni hiyo imekuwa ikikaidi kulipa ushuru wa asilimia tano ya gharama ya kila nguzo ambapo ushuru huo umefikia Sh  bilioni 2.9 hali iliyopelekea uongozi wa mkoa kuzuia nguzo hizo zisitoke.

Wiki iliyopita akiwa katika ziara ya Mkoa Ruvuma, Waziri Mkuu alipokea malalamiko kuhusu mkoa wa Iringa kuzuia kusambazwa kwa nguzo za umeme ndipo alipoamua kuwaita Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi pamoja na wakuu wa wilaya, wakurugenzi pamoja na wenyeviti wa halmashauri wanaotoka katika wilaya zinazozalisha nguzo.

Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemevu, Jenista Mhagama, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Josephat Kandege, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya pamoja na maofisa wengine wa Serikali.

Alisema lengo la kikao hicho lilikuwa kupata ufafanuzi kuhusu malalamiko yaliyotolewa dhidi ya uongozi wa Mkoa wa Iringa kuhusu kuzuia usafirishaji wa  nguzo za umeme zinazotumika kwenye miradi ya nishati ya umeme vijiji (REA).

Baada ya kupata maelezo hayo, Waziri Mkuu alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Iringa kuiandikia bili kampuni ya New Forest ili ilipe ushuru huo kuanzia Julai 2018 walipoanza kusambaza nguzo.

Asilimia 90 ya nguzo za umeme nchini zinatoka Iringa. Tanzania ina  viwanda tisa vya kutengeneza nguzo na kati ya viwanda hivyo vinane vipo Iringa na kimoja kipo Tanga.

Kampuni ilizuiwa kutoa nguzo ndani ya mkoa wa Iringa tangu Novemba 2018 hadi Januari 2019 huku ikitakiwa kulipa ushuru wa asilimia tano ya gharama ya kila nguzo ambapo ilikaa ikitaka iendelee kulipa Sh 5,000 kwa kila nguzo kama walivyokubaliana na TANESCO jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Hata hivyo, nguzo za umeme ambazo zilikuwa zimezuiwa kwa muda mrefu katika maeneo ya uzalishaji hususani mkoani Iringa na kusababisha kukwama kwa baadhi ya miradi ya usambazaji umeme kwenye baadhi ya mikoa nchini juzi zimeanza kusambazwa huku taratibu nyingine za malipo zikiendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles