24.6 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

RC Dodoma apiga marufuku kamari

RRAMADHAN HASSAN-DODOMA

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge amegeuka mbogo kwa wachezesha kamari ambapo  amepiga marufuku uchezeshwaji wa kamali katika nyumba yoyote mkoani humo.

Marufuku hiyo imekuja kutokana na Jeshi la Polisi mkoani hapa kufanya msako na kkamata mashine 77 za kuchezeshea kamari zikiwa hazina vibali pamoja na kutosajiliwa pamoja na kufungwa majumbani hali ambayo imewafanya baadhi ya watoto kushindwa kwenda shule na kuanza kucheza.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini hapa, Dk.Mahenge alisema ni marufuku kamari kuchezwa kmajumbani  na badala yake ichezwe katika Klabu ama kumbi za starehe.

“Sasa hivi hata majumbani wachina wanafunga mashine wanaanza kuchezesha hii inawafanya watoto wetu wasahau kabisa shule.

“Napiga marufuku kwa mtu yeyote kufunga mashine za kamari katika nyumba na kama unayo ikabidhi mwenyewe kwa kuileta ili usije ukapata shida,narudia tena tutakuja kuonana wabaya sitaki kusikia mashine za kamari zimefungwa nyumbani,” alisema.

Pia mkuu huyo wa mkoa aliitaka Bodi ya michezo ya kubahatisha waende Mkoani humo ili wakazikague mashine hizo.

“Bodi ya Bahati nasibu njooni mzikague hizi mashine maana kwa sasa zimefungwa kiholela kila sehemu na wachina hii ndio imekuwa biashara yao tunaharibu kizazi cha sasa na cha baadae,” alisema.

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wazazi na walezi kufuatilia maendeleo ya watoto wao kama wanafika shuleni kwani anazotaarifa kuna baadhi hawafiki na wamekuwa wakienda kucheza kamari.

“Uzalendo ndio kila kitu,niwaombe wazazi kuwafuatilia watoto wao kwani baadhi wamekuwa hawafiki shule na wengine wakicheza kamali katika maeneo mbalimbali hili sitaki litokee tena,” alisema Dk.Mahenge.

Mwisho     

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles