24.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi yapiga marufuku ufyatuaji fataki mwaka mpya

Na AMINA OMARI- TANGA

JESHI la Polisi mkoani Tanga limepiga marufuku ufyatuaji wa fataki na milipuko ya aina yoyote pamoja na kurusha mawe katika paa za nyumba katika mkesha wa mwaka mpya. 

Kamanda wa MKoa huo, Edward Bukombe aliyasema hayo jana wakati akizungumzia namna walivyojipanga katika kuimarisha usalama mkoani humo. 

Alisema kuwa iwapo milipuko hiyo itafyatuliwa kiholela inaweza kusababisha majanga ya moto yanayoweza kusababisha uharibifu wa mali na kugharimu maisha ya watu.

Aliongeza kuwa mwananchi atakayekamatwa akijaribu kufanya vitendo hivyo atakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za sheria. 

“Jeshi linatoa wito kwa wakazi wa Tanga wanapokwenda kwenye sherehe za mwaka mpya kuhakikisha nyumba zao zinabaki na uangalizi ili kuepuka wizi unaoweza kutokea”.alisema Kamanda Bukombe. 

Hata hivyo alisema kuwa jeshi hilo limejipanga kuendesha doria katika mitaa yote ili kuhakikisha hakuna vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyoweza kufanyika katika mkesha huo. 

Aidha Kamanda Bukombe aliwataka wamiliki wa vyombo vya moto kutokiuka kanuni za usalama barabarani  na kuendesha vyombo hivyo kwa mwendokasi au wakiwa wamelewa. 

“Niwatake kila anayeendesha chombo cha moto azingatie sheria za usalama hasa kipindi hiki cha kuelekea kwenye sikukuu atakayekaidi atawajibishwa kisheria”alisema 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles