30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi yamtaja aliyejilipua shambulizi la Nairobi

NAIROBI, KENYA

JESHI la Polisi nchini hapa limetangaza kumtambua mtu aliyejitoa mhanga kwa kujilipua na bomu katika shambulizi la kigaidi lililofanyika katika Hoteli ya Dusit D2 na kusababisha vifo vya watu 21.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, taarifa ya polisi ilisema kuwa mtu aliyejilipua kwa bomu ni kijana mwenye umri wa miaka 25 na mpiganaji wa kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab aitwaye Mahir Khalid Rizik.

Polisi walisema Mahir alizaliwa na kukulia mjini Mombasa na anadaiwa kurejea nchini hapa Januari 13, mwaka huu kutoka Somalia alikokuwa mafunzoni tangu mwaka 2018.

KIAMBU

Kurejea kwake kunahusishwa na mtuhumiwa mwingine, Ali Salim Gichunge anayefahamika kwa jina jingine la Farouk, aliyerejea na kuweka makazi Muchatha katika Kaunti ya Kiambu.

Pia polisi wanaamini kuwa walibadilishwa misimamo na imani na Ramadhani Hamis wa Al Shabaab anayesadikiwa kuishi Somalia.

Kikosi cha kupambana na ugaidi kimesema kuwa Mahir amewahi kuhusika katika mashambulizi yaliyolengwa katika vituo vya vyombo vya ulinzi na usalama na aliwahi kwenda Somalia.

Picha za video za eneo la tukio katika Hoteli ya Dusit zimeonesha kuwa gaidi huyo alikuwa anatembea kuelekea sehemu ya kujihudumia kabla ya kujilipua.

Ripoti za polisi zinasema kuwa mhanga huyo alisababisha vifo vya watu sita.

Pia wanaamini Mahir alikodi chumba katika hoteli hiyo huku akiwasiliana na magaidi wenzake wakati wakielekea kufanya hujuma hiyo.

Watuhumiwa sita wanaohusishwa na tukio hilo wamekamatwa na polisi, kati yao watano watawekwa rumande kwa siku 30 wakati uchunguzi unaendelea.

Wakati huohuo, kikosi cha upelelezi cha polisi jana kilimkamata baba wa mtuhumiwa huyo katika Mtaa wa Majengo huko Mombasa pamoja na mkewe aliyekamatwa huko Bakarani kwa lengo la kuhojiwa na vyombo vya usalama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles