22.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Polisi afia baa

PNA AMON MTEGA

-SONGEA

ASKARI Polisi, Konstebo Donald Motoulaya (29) wa ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, amekutwa amefariki dunia akiwa baa ya Friends Pub mjini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Marwa alisema tuko hilo limetokea juzi Machi 13, saa 4:30 usiku.

Alisema Motoulaya kabla ya kifo hicho, alikuwa ameenda kwenye baa hiyo kwa ajili ya shughuli zake binafsi .

Alisema wakati anaingia mlangoni alijikwaa kwenye ngazi na kuanguka, kisha akatolewa nje na mhudumu wa baa hiyo, Jaibu Nyoni (26).

Alisema askari huyo alifika kwenye baa hiyo, wakati akitokea baa nyingine ya Yapenda au Mtini Pub kwa lengo kujipatia kinywaji.

“Baada ya kutolewa nje, huku mhudumu akiendelea na shughuli zake, askari huyo alijipenyeza  na kuingia chumba cha ndani, kisha kwenda kukaa kwenye kochi kutokana na askari huyo kuzoea mazingira ya maeneo hayo bila wahudumu kutambua kama alikuwapo ndani,” alisema Kamanda Marwa.

Alisema wahudumu  walibaini kuna mtu amekaa kwenye kochi na haamki walipokuwa wakifanya usafi ndipo wakatoa taarifa kituo kuu cha polisi cha mji Songea na polisi walipokwenda walibaini amefariki dunia.

Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Homso mjini Songea ukisubiri taratibu nyingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,415FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles