24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Pochettino: Tottenham ubingwa tusahau

LONDON, ENGLAND

BAADA ya juzi timu ya Tottenham kukubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Chelsea kwenye michuano ya Ligi Kuu England, kocha wa timu hiyo, Mauricio Pochettino, ameweka wazi kuwa haiwezekani wakatwaa ubingwa msimu huu.

Kocha huyo amedai itakuwa ngumu kuweza kushindana na Manchester City na Liverpool ambao wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

Kabla ya kichapo hicho cha juzi, mwishoni mwa wiki iliyopita Tottenham ilijikuta ikipoteza mchezo wake dhidi ya Burnley kwa mabao 2-1, hivyo kumkatisha tamaa kocha huyo kutwaa ubingwa.

Hata hivyo, kutokana na hali hiyo ya kupoteza baadhi ya michezo, kocha huyo ameweka wazi kuwa, Tottenham wana safari ya miaka mitano hadi 10 kuweza kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu England.

“Kwa haraka naweza kusema tumepoteza, tumefanya makosa na kupoteza mchezo, ukweli ni kwamba hatujacheza kwenye kiwango chetu.

“Chelsea walipata nafasi moja ya kupiga shuti lililolenga lango na kufanikiwa kupata bao, lakini sisi hatukuweza kulenga lango, hivyo naweza kusema ni ngumu kuwa bingwa wa ligi kwa namna hiyo.

“Baada ya kupoteza katika mchezo dhidi ya Burnley, nilisema wenzetu walikuwa wagumu, leo (juzi) tumekutana na upinzani mwingine ambao unatufanya tuzidi kuwa katika wakati mgumu wa kuwakuta Man City na Liverpool.

“Kwa sasa tunapambana kwa ajili ya kushinda michezo yetu na si kutwaa ubingwa, lakini wao wanapambana kwa ajili ya ubingwa,” alisema kocha huyo.

Kwa sasa Tottenham wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi huku wakiwa na pointi 60, baada ya kucheza michezo 28, wakati huo Manchester City wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 68 huku Liverpool wakiwa nafasi ya kwanza kwa pointi 69.

Kesho Tottenham watakuwa kwenye uwanja wa nyumbani na kuwakaribisha wapinzani wao Arsenal kwenye mchezo wa Ligi Kuu. Timu hizo zinatofautiana kwa pointi nne, Arsenal wanashika nafasi ya nne wakiwa na pointi 56.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles