27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

Papa Francis atangaza sheria mpya ya kanisa

VATICAN CITY, VATICAN

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, ametangaza kanuni mpya zinazowataka mapadri wote, watawa na viongozi wengine wa kanisa hilo kuripoti matukio ya unyanyasaji wa watoto kingono au kufichwa kwa wakuu wa kanisa hilo kuhusu makosa ya namna hiyo lakini si mamlaka za kiraia.

Papa amefafanua kwamba taarifa za matukio hayo yaripotiwe kwa maaskofu wa mitaa. Lakini ikiwa mtuhumiwa huyo ni Askofu, Kardinali au kiongozi mwingine wa ngazi za juu kanisani, basi makao makuu Vatican yanapaswa kujulishwa.

Kanuni hizo zilizotangazwa juzi zinatarajiwa kuanza kutekelezwa Juni mosi mwaka huu. Kanisa Katoliki limekuwa likilaumiwa kwa miaka mingi kuhusu visa vya unyanyasaji wa kingono unaofanywa na wachungaji wake duniani kote dhidi ya watoto na makao makuu ya Vatican mara kwa mara yamekuwa yakiahidi kushughulikia tatizo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles