24.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 8, 2022

Nyuki kufungwa hifadhini kuzuia wanyama kutoroka

Na BENJAMIN MASESE-MWANZA

SERIKALI  imeitaka bodi mpya ya Ushauri ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS)  kuhakikisha inaanzisha utaratibu wa ufugaji  nyuki pembezoni mwa hifadhi za taifa  ili kuepusha wanyama wasitoroka na kuingia kwenye makazi ya watu.

Imesema  ufugaji huo utasaidia Serikali kuhifadhi misitu bila kutumia mitutu ya bunduki kutokana na baadhi ya wananchi kuvamia maeneo hayo sambamba na kupata asali  kwa kuwa soko la bidhaa lipo kwa uhakika ndani na nje ya nchi.

Kauli  hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Waziri  wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangala alipokuwa akizindua Bodi mpya ya TFS jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

Alisema ufugaji nyuki itakuwa na manufaa makubwa kwa kila upande ikiwamo ajira na uchumi wa nchi.

Dk. Kigwangala  alisema ikiwa asali  itakuwapo kwa wingi wawekezaji wa bidhaa zitokanazo na bidhaa hiyo watakuja nchini huku akishauri kuwapo mkakati kababe wa nchi nzima kuwezesha wananchi kwenye ufugaji huo.

“Tumekuwa tukisikia wanyama wanavamia makazi ya watu kila mara na kusababisha vifo na  uharibifu wa mashamba, wazo ambalo naliona na nataka TFS mwone kuna umuhimu wa kulifanyia kazi ni kufuga nyuki kwa kuzungukia hifadhi zote za wanyama na misitu.

“Sote tunajua Rais John Magufuli ameagiza kuangalia wale watu wanaoishi karibu na hifadhi  tuone namna gani tunawarasimisha ingawa si wote.

“Mchakato huo unaendelea kutembelea maeneo hayo lakini baada maeneo hayo kutenganishwa na kumaliza  suala hilo ni vema tukaanzisha ufugaji wa nyuki  kwa kuweka mzinga eneo lote.

“Pia tuwashirikishe wananchi hata kwa kuwawezesha nao wafuge kwani soko lipo, ikiwa tutafanikiwa tutakuwa tumepata suluhisho la wanyama kutoroka hifadhini na watu kuvamia misitu yetu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,235FollowersFollow
549,000SubscribersSubscribe

Latest Articles