24.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

NSSF yasaidia mashine Hospitali ya Temeke

Na CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umetoa msaada wa mashine 12 za kupimia shinikizo la damu (BP),  kwa uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke.

Akikabidhi msaada huo jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa NSSF Temeke, Barnabas Ndunguru, alisema msaada huo wenye thamani ya zaidi ya Sh milioni tano, ni sehemu ya fadhila za shirika hilo kwa wateja wake na jamii kwa ujumla.

Alisema NSSF ina wanachama zaidi ya 4,000 ambao wanapata huduma katika hospitali hiyo, hivyo mashine hizo zitasaidia kuchangia huduma ya natibabu kuwa bora zaidi.

“Msaada huu ni imani yetu utapunguza changamoto zilizopo sasa za uhaba wa vifaa tiba katika hospitali hii ambapo nasi kama wadau tuliletewa ombi na uongozi wa hospitali tukaamua kuchangia mashine hizi,” alisema Ndunguru.

Alisema katika kipindi hiki cha Maonyesho ya Sabasaba, wamejipanga kutoa huduma za matibabu, kupima afya na kuandikisha wanachama wapya.

Kwa upande wake, Katibu wa Afya wa Hospitali hiyo, Lilian Mwanga, alisema hospitali hiyo inakabiliwa na uhaba wa vifaa tiba, ikiwamo mashine za shinikizo la damu.

Alisema kwa sasa wananchi wengi wanakabiliwa na changamoto ya magonjwa ya shinikizo la damu, hivyo kigunduzi pekee ni mashine hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles