24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Neema kwa wakulima

IBRAHIM YASSIN-SONGWE

NAIBU Waziri wa Kilimo, Maji na Mifugo, Omari Mgumba, amewataka wakulima kutumia mbinu sahihi za kilimo ili kuongeza tija kwa kuzingatia afya ya udongo huku akikiri kutokuwepo kwa matumizi ya pembejeo zisizo na tija zikiwemo mbolea ambazo haziendani na udongo uliopo.

Mgumba aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Isansa wilayani Mbozi, ukilenga kuzindua upimaji wa afya za udongo mkoani Songwe kwa lengo la kumwezesha mkulima kulima kilimo chenye tija.

Alisema wakulima wanapaswa kuinua hali ya uchumi kupitia kilimo kwa kufuata taratibu na njia bora za kilimo ambapo Serikali imekusanya sampuli kwa ajili ya kufanya tafiti na kupima udongo ambapo pia alisema mafunzo yatafanyika katika maeneo yaliyofanyiwa tathmini.

“Tathmini inafanyika katika wilaya 16 ikiwemo Songwe, tupo hapa leo kuzindua mafunzo ya upimaji wa udongo wa ufadhili wa Kampuni ya Mbolea ya OCP Afrika yenye makao makuu nchini Morocco, lengo ni kuongeza tija na kuongeza thamani ya kilimo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles