28 C
Dar es Salaam
Monday, January 24, 2022

Mwanamuziki wa Rwanda asitisha ziara yake Burundi

KIGALI, RWANDA

MWANAMUZIKI maarufu nchini Rwanda, Ngabo Medard Jobert maarufu kama Meddy, amelazimika kusitisha ziara yake ya kimuziki katika nchi jirani ya Burundi kwa sababu za kiusalama.

Kwa mujibu wa Idhaa ya Kiswahili ya Ufaransa, RFI, imesema mwanamuziki huyo alitarajiwa kuwaburudisha wafuasi wa muziki wake jijini Bujumbura mwishoni mwa wiki hii, na sasa ziara hiyo kwa mujibu wa meneja wake, itafanyika wakati mwingine.

Taarifa hiyo imeoneza kuwa uamuzi wa mwanamuziki huyo umechangiwa na hali iliyopo sasa ya uhusiano kati ya nchi hizi mbili kuwa mbaya hivyo kuzua hofu  za kiusalama.

Serikali ya Bujumbiura inawatuhumu viongozi wa Rwanda hususani Rais Paul Kagame mwenyewe kuwa wanaingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo na kufanya kila wawezalo ili kumuondoa madarakani Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.

Madai ambayo Rwanda imetupilia mbali na kusisitiza kuwa tuhuma zinazotolewa na serikali ya Burundi ni mbinu za kutaka kujihusisha na mauaji ya kimbari dhidi ya wapinzani wake.

Zaidi ya raia wa Burundi 250,000 wamekimbilia nchi jirani ikiwezo Rwanda, kufuatia kuzuka kwa machafuko na mivutano ya kisiasa nchini Burundi.

Machafuko nchini Burundi yalianza mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka 2015 kufuatia hatua ya Pierre Nkurunziza ya kugombea tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu.

Licha ya kutekelezwa jitihada za kimataifa kwa minajii ya kuhitimisha mgogoro wa Burundi, lakini juhudi hizo hadi sasa zimeshindwa kuzaa matunda.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
176,415FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles