21.9 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Mwalimu jela miaka 30 kwa kubaka mwanafunzi

Na SAMWEL MWANGA-MASWA

MAHAKAMA ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, imemhukumu Mwalimu Abubakari Katakweba (32) wa Shule ya Msingi  Mwafa wilayani humo, kwenda jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa kidato cha pili (jina limehifadhiwa).

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Fredrick Lukuna, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kutoa adhabu hiyo.

Hakimu Lukuna alisema mashahidi wote waliofika mbele ya mahakama hiyo walieleza jinsi mshtakiwa huyo ambaye ni mwalimu alivyofanya  kitendo hicho, ikizingatiwa ni mlezi au mzazi  wa wanafunzi wote.

Hata hivyo, mshtakiwa baada ya kutiwa hatiani, aliiomba

mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ndilo kosa lake la kwanza na pia ana familia ambayo inamtegemea.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka ambaye ni Mkaguzi wa Polisi, Nassib  Swedy, kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 10,

mwaka huu katika Kijiji cha Hinduki wilayani humo.

Mwendesha Mashtaka Nassib alieleza mahakama hiyo kuwa siku ya tukio saa 1:00 jioni, mshtakiwa akiwa katika eneo lenye vibanda vya biashara katika kijiji hicho, alimwita mwanafunzi huyo wa Shule ya Sekondari Sukuma.

Alisema kwa kuwa mwanafunzi huyo alimfahamu mshtakiwa kuwa ni mwalimu, alikwenda lakini ghafla alimshika mkono na kisha kumfumba mdomo kwa mkono wake ili asipige kelele na kumwingiza katika chumba ambacho kilikuwa kikitumika kunyolea nywele (saluni) na kisha kumvua ngua na kuanza kumbaka.

Mwendesha mashtaka huyo alisema kitendo hicho ni kinyume  na kifungu 130(1)(2) na kifungu 131(1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,719FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles