25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Mo aongeza mzuka Simba

ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

MWEKEZAJI wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, ameongeza mzuka ndani ya timu hiyo akiwataka mashabiki na Watanzania kujitokeza kwa wingi kuwasapoti wachezaji katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe, utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mo, alisema kujitokeza kwa mashabiki kuna faida kuu mbili, mojawapo ni kuongeza nguvu kwa wachezaji huku wakiamini kuwa Watanzania wapo nyuma yao, lakini pili inasaidia kuwaogopesha wapinzani.

“Nawaomba sana mashabiki ikitokea bahati mbaya ya hapa na pale, tuendelee kushabikia si tu mpaka tukipata bao, naomba sana tubadilike kwenye hilo, tushangilie Simba tangu mwanzo hadi mwisho na niwahakikishie wachezaji wetu wanaweza kutupa furaha kesho (leo) kwa kuwafunga si chini ya mabao mawili bila,” alisema Mo.

“Shabaha yetu si tu kufanikiwa mwaka mmoja, tunataka kushinda kombe kila mwaka ili tushiriki Ligi ya Mabingwa kila mwaka, tunataka kushinda Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika, mimi naamini uwezo tunao, tumtangulize Mungu lakini pia tujenge kikosi kitakachopambana na timu yoyote kubwa Afrika,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles