28.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Mbowe, Matiko wapokewa kwa shangwe bungeni

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

BAADA ya kutoka gerezani walikokaa kwa zaidi ya miezi mitatu, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko( Chadema), jana walishangiliwa na baadhi ya wabunge huku Spika wa Bunge, Job Ndugai akichombeza kwa kudai kwamba  walikuwa Mtera.

Machi 7, mwaka huu, Mahakam Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliwarejeshea dhamana Mbowe na Matiko, baada ya kushinda rufaa waliyoikata wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Kisutu.

Jana majira ya saa 11.23 asubuhi wakati wakiingia ukumbi wa Pius Msekwa jijini hapa kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa uwasilishwaji wa mapendekezo ya Serikali ya mpango wa maendeleo wa Taifa na ya kiwango na ukomo wa bajeti ya Serikali kwa mwaka 2019/20 wabunge hao walishangiliwa na wenzao, huku baadhi wakiwakumbatia.

Mara baada ya kuingia akina Mbowe baadhi ya wabunge walianza kuimba na kupiga makofi.

Wakati Spika Job Ndugai, akimkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alichombeza kwa kuwakaribisha Mbowe na Matiko bungeni huku akidai kwamba kwa lugha ya kibunge walikuwa Mtera.

“Lakini Mheshimiwa Waziri Mkuu nianze kwa kumtambua kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni Mheshimiwa Freeman Mbowe na Matiko kwa lugha ya kibunge tunasema walikuwa Mtera hivyo karibuni kutoka Mtera,”alisema Spika Ndugai huku wabunge wakishangilia.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kabla ya kuanza kuongea naye aliwakaribisha bungeni na kusema ni matumaini yake Mungu atasaidia wahudhurie kwa kadri inavyotakiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,908FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles