28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Matatizo mengi ya benki ni ya kujitakia

Shermarx Ngahemera

WAHENGA wanasema kuwa adui wamtu au sumu ya mtu ni mtu mwenyewe kwani  kupanda au kuharibika kwa mtu ni matendo yake na vivyo kwa taasisi kuwa imara  kwani  mara chache sana tatizo hupachikwa ila hutokana na mwenendo wake mhusika.

Kufanikiwa kwa mabenki makubwa mawili ya NMB Plc na CRDB Plc inatokana na mabenki hayo kwenda na wakati na kuzingatia ushauri wa kitaalamu wa kufuata mahitaji ya soko kama inavyotaka. Kile mwanzoni kilichukuliwa kama ongezeko la gharama za uendeshaji sasa kimekuwa kichocheo cha faida na upanuzi wa wigo wa mabenki hayo. Mabenki ni wateja na kama huna huwezi kukwepa kupata hasara.

Ushauri wa wazi ulitolewa na bado kuwa ni kweli  ni kuwa benki zibadilike katika utoaji huduma kwa kutumia sana bidhaa za kiteknolojia na kupeleka huduma kwenye  jamii za pembezoni ambazo hazina huduma hiyo, kulegeza masharti ya kuendesha akaunti za wateja, kupunguza riba na ikibidi kutafuta dhamana nyingine zaidi ya mali zisizohamishika.

Azimio la Maya 

Azimio la Maya ni lile ambalo mataifa zaidi ya 60 katika nchi zinazochipukia kiuchumi  Duniani kama Tanzania ambazo zilikaa na kuweka nia kuwa lazima wafungue milango kwa watu  zaidi ya bilioni mbili duniani kwa kuwashirikisha katika masuala ya fedha.

Maamuzi haya yalifanyika katika mkutano uliofanywa Maya Rivera nchini Mexico ili kufanya juhudi ya ushirikishi wa watu walio nje ya mifumo rasmi ya kibenki kujiunga nayo ili waweze kupata stahiki zinazotokana na mtu kuwa na akaunti ya kibenki au huduma ya fedha na hivyo kufaidika.

Mategemeo ni kufungua uwezo wa watu hao katika masuala ya kijamii kipesa na kiuchumi kutaleta mabadiliko ya msingi ya maisha na kufuta umasikini duniani na mabenki nayo kusitawi vilivyo.

Tanzania kama nchi imepiga hatua kubwa sana katika suala la ushirikishi wa wananchi (inclusiveness) wake katika masuala ya fedha na kuongoza watu wanaoishi katika eneo hili la Afrika Mashariki kutokana na utafiti wa Fintech.

Hayo yanatokana na sera nzuri za serikali kuhusu suala hilo na msimamo thabiti wa Benki Kuu kuhusu  kutekeleza  mahitaji  mapana ya Azimio la Maya kwa upanuzi wa shughuli za kibenki nchini;  kwa kuruhusu shughuli nyingine zifanywe na taasisi ambazo sio za kifedha kama makampuni ya simu nay ale ya usafiri.

Hivi basi milango ikafunguliwa kwa  M-Pesa, Tigo Pesa , Airtel Money,  na Easy Pesa ambazo kimsingi ni kampuni za mawasiliano lakini zinafanya huduma za fedha na kibenki kwa kuanzisha majukwaa ya kuendeshea masuala ya kibenki na fedha na hivyo kupanua kwa marefu na mapana huduma hizo na wengi kufaidika.

Mwenendo wa baaadhi ya mabenki kuunga mkono na wengine kukataa mwenendo na wazo zima la ushirikishi kwa kuanzisha  bidhaa za kibenki  za kushughulikia masuala hayo na hivyo wachambuzi wanasema hatma ya benki hizo sio nzuri kwani hazitafanikiwa kupanuka na kukosa wateja wa wazi.

Kwa kuzingatia umuhimu wake katika uchumi wa Tanzania na walalahoi wake hususan wanaoishi vijijini ambako kipato chao ni duni njia pekee kwa mabenki mwelekeo wake uwepo kwenda vijijini kukamata soko hilo la watu bilioni 2 duniani. Asiyefanya hivyo ni kosa kubwa na soko litamwadhibu na sio vinginevyo kwani mteja ni mfalme popote alipo.

Shirika la Fedha Duniani (IMF) lilitabiri kuwa mwaka   2013-2017, kungekuwapo uimara wa mambo ya fedha na hivyo ukuaji wa Uchumi. Kweli ilifanyika na kukawa na uimara nchini Tanzania.

Mwishoni mwa Mwaka 2013 Serikali ilianzisha  Mfumo wa Taifa wa Ushirikishwaji  Kifedha (National Financial Inclusion Framework (NFIF) awamu ya kwanza 2014 hadi 2016 kama  sehemu ya utekelezaji  wa Azimio la Maya  ambalo lilikuwa ni kutoa ushirikishi kwa kujifunga na hali ya kuongeza ushiriki wa Watanzania  watu wazima  kujiunga na mifumo rasmi ya Fedha  ili ufikie kiasi cha asilimia 75 ndani ya miaka 6. 

Lengo limefikiwa na kupitwa na mabadiliko yameanza kuonekana kwenye jamii kwa kuzipokea benki huko waliko na wao mabenki kuanzisha mpango wa uwakala kila mahala na hivyo kupanua wigo wa biashara zao.

Mwenendo  huo wa Fedha umetekelezwa kwa miaka mitatu 2014  hadi  2016  chini ya uangalizi wa  Baraza la Taifa la Ushirikishwaji Masuala ya Fedha (Financial Inclusion National Council (FINCO)   ambayo ni bodi  ya taasisi  11 kutoka  taasisi na Wizara za Serikali  ikiwamo  pia Benki Kuu ya Tanzania , Wizara ya Fedha , na Mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania (TCRA) kama washiriki wakuu. 

Mabenki yanayopata matatizo ya ukata sasa nchini ni yale ambayo yamekaidi kufuata ushauri mzuri wa dunia kupitia Azimio la Maya na watekelezaji wazuri kama NMB Plc wanaongoza kwa kukua na upatikanaji faida nchini.

Mfumo wa Taifa wa Ushirikishwaji  Kifedha (National Financial Inclusion Framework (NFIF) na Baraza la Taifa la Ushirikishi Masuala ya Fedha (Financial Inclusion National Council (FINCO)  na hivyo kunufaisha taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles