23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Marekani yaongeza ushuru bidhaa za China

WASHINGTON, MAREKANI

SERIKALI ya Marekani imetangaza kuongeza kiwango cha ushuru kwa bidhaa zote zinazotoka China na kuingia nchini humo kupitia miji mbalimbali.

Nyongeza ya ushuru wa dola bilioni 200 kwa bidhaa za China zinazoingia nchini Marekani imetangazwa na Rais Donald Trump wa nchi hiyo na imeanza kutekelezwa jana, hatua ambayo inatarajiwa kuongeza mvutano kati ya Marekani na China.

Utawala wa Rais Trump uliongeza ushuru wa bidhaa hizo kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25. China tayari imetishia kulipiza kisasi ikiwa Trump ataendelea na kitisho chake cha kuongeza ushuru, lakini haijafafanua hatua itakazochukuwa.

Nyongeza hiyo ya ushuru imeanza kutekelezwa licha ya wajumbe wa Marekani na China kuanza tena mazungumzo ya kibiashara juzi ambayo yanafanyika mjini Washington na kuendelea hadi leo.

Makamu wa rais wa China, Liu He, anayeshiriki mazungumzo hayo amesema nyongeza hiyo itakuwa na athari ulimwenguni kote. Timu ya Trump inaimarisha vita yake kibiashara na China ambayo inadai inazorotesha ahadi ilizotoa katika mazungumzo yao ya awali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles