27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mama aua watoto wake sita kwa mapanga

MURUGWA THOMAS -NZEGA

MAMA mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Nana Maganga (35), mkazi wa Kijiji cha Luzuko Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, anadaiwa kuwauwa watoto wake sita kwa kuwakatakata kwa mapanga, huku naye akiuawa na wananchi wenye hasira.

Tukio hilo lilitokea jana saa 11 alfajiri ambapo inadaiwa mama huyo ambaye alikuwa mgonjwa wa akili, aliwauwa watoto wake wa kuzaa watano pamoja na mmoja wa kaka yake, huku wengine wanne wakijeruhiwa katika tukio hilo la kinyama.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley, alisema mauaji hayo ya watoto yalifanywa na mama yao, huku watoto wengine wanne wakijeruhiwa.

Kamanda Nley alisema Nana, alikuwa ni mgonjwa wa akili hivyo alikwenda kwa mganga wa jadi ambaye ni shemeji yake kwa lengo la kupatiwa matibabu, ndipo mkasa huo wa kusikitisha ulipotokea na kuua watoto wake ambao walikuwa wamelala chumba kimoja.

Alisema baada ya kufanya mauji hayo wananchi walisikia kelele na kulazimika kuizunguka nyumba hiyo na kufanikiwa kumdhibiti mama huyo kwa kumfunga kamba mikononi na baada ya muda alifariki dunia kwa kile kinachodaiwa ni kipigo.

Hata hivyo alisema baada ya Polisi kufika kwenye eneo la tukio walihoji mashuhuda ambao walidai kuwa kifo cha mama huyo kimetokana na kunywa sumu yeye mwenyewe jambo ambalo si kweli.

Kutokana na hali hiyo Kamanda huyo wa Polisi, alisema wanawashikiliwa watu watano akiwamo mume wa mama huyo na mganga wa jadi kwa tuhuma za mauaji ya Nana.

Alisema  kuwa upelelezi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini nini hasa chanzo cha mauaji hayo ya watoto wadogo.

Aliwataja watoto hao waliouawa kuwa ni pamoja na Pala Massanja(3),  Shija Dotto (2), Nyawele Dotto(2), Sida Dotto(5), Kulwa Dotto (4) na Dotto  Dotto (4) .

Watoto wanne waliojeruhiwa ni Kundi Dotto, Nembwa Dotto, Milembe Massanja pamoja na Mwashi Massanja.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nzega , Godfrey Ngupulla,  alisema tukio hilo limeibua hisia kali kwa wananchi kwani haijawahi kutokea mauaji ya mama kuuwa watoto wake na kuwataka  wananchi kuwapeleka hospitali wagonjwa wa akili ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

Ngupulla alisema mgonjwa huyo huenda alitumia dawa nyingi za mitishamba hadi kusababisha kuchanganyikiwa na kuanza kushambulia watoto na hatimaye kusababisha mauaji hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles