23.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 10, 2022

Mafuriko yateketeza miji na vijiji Iran

TEHRAN, Iran 

MAELFU  ya miji na vijiji  yameteketezwa na mafuriko yaliyoyakumba maeneo ya Kusini  mwa nchi hii na serikali imetahadharisha kutokea mengine katika mpaka na Irak ambako kuna mabwawa na mito mingi.

 Mafuriko hayo ambayo yalianza tangu mwezi Machi mwaka huu yameshasababisha vifo vya watu 70 na kuaribu miundo mbinu  na kuwalazimisha  maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao katika maeneo mbalimbali nchini hapa.

Mapema mwishoni mwa wiki iliyopita Maofisa wa Irak walilazimika kufunga mpaka wa  Chazabeh, baada ya serikali ya hapa kupiga marufuku safari na biashara katika Jimbo la  Khuzestan lililopo Kusini mwa nchi hii kutokana na wasiwasi wa kutokea mafuriko zaidi.

Shirika la Habari nchini hapa, IRNA, liliripoti jana kwamba Mamlaka ya Mapato katika Jimbo hilo la  Khuzestan, katikati mwa wiki iliyopita liliziagiza  kampuni za biashara kutumia mpaka mwingine badala ya huo wa Kusini mwa nchi.

“Mito yetu na mabwawa yamejaa maji kwa asilimia  95 na tunatarajia kuibuka kwa mafuriko mengine,”ilieleza taarifa ya mamlaka hiyo.

 “Barabara zote za usafirishaji zinazopitia karibu na mto wa  Karkheh,zinatarajia kujaa maji na sisi kama mamlaka husika tunaagiza zichukuliwe hatua za dharura ili kukabiliana na wingi wa maji,”iliongeza taarifa hiyo.

Eneo hilo la Jimbo la Khuzestan, lina mito mikubwa mitatu ambayo inakatika katika vijiji na miji kadhaa  ukiwamo mto wa Karoun ambao unapitia katika Jimbo la Ahvaz.

Waziri wa Mambo ya Ndani,  Abdoreza Rahmani Fazli anasema kwamba mafuriko hayo yatakuwa yamewathiri watu wapatao 400,000  kati ya zaidi ya milioni 4.7 wanaoishi katika Jimbo hilo la Khuzestan.

Alisema jana  kwamba mafuriko mengine yanatarajiwa kuyakumba maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa nchi ukiwamo mji wa  Mashhad.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,395FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles