24.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 8, 2022

Kusaga amshukuru JPM, asifia wasifu wa Kibonde


Elizabeth Joachim, Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group (CMG), Joseph Kusaga amemshukuru Rais Dk John Magufuli kwa ushirikiano aliouonyesha kwenye matukio ya misiba iliyoikumba kampuni hiyo ukiwemo wa aliyekuwa mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi Clouds Media, Ruge Mutahaba pamoja na aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha Jahazi, Ephraim Kibonde .

Kusaga ametoa shukurani zake hizo leo Jumamosi Machi 7 Jijini Dar es Salaam katika makaburi ya Kinondoni wakati wakimuhifadhi Ephraime Kibonde kwenye nyumba yake ya milele.

“Natoa shukrani zangu za pekee kwa Rais wetu Dk John Magufuli kwa kuonyesha ushirikiano katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na ndugu zetu, nimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, Wasanii,wanatasnia ya vyombo vya habari na Ndugu pamoja na familia katika kipindi hiki kigumu.

“Kiukweli ni kwamba Kibonde alikuwa mtangazaji wa tofauti sana kwa kuwa kila kipindi alifanya ikiwemo michezo, habari, Mc na mengine mengi sijui kama atatotekea mtangazaji kama Kibonde,” amesema Kusaga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,235FollowersFollow
549,000SubscribersSubscribe

Latest Articles