23 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Kocha AS Vita aivulia kofia Simba

MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM

BAADA ya kuchapwa mabao 2-1 na Simba katika mchezo wa mwisho wa kundi D, Kocha Mkuu wa AS Vita, Frolent Ibenge, amekiri wazi kuwa wapinzani wao walikuwa bora katika mechi hiyo ambayo walicheza vizuri na walistahili kushinda.

AS Vita ilijikuta ikikumbana na kichapo hicho kulichowafanya kushindwa kutinga robo fainali, baada ya kumaliza mkiani mwa msimamo wa kundi hilo ikiwa na pointi saba katika michezo yake sita waliyocheza kwenye michuano hiyo.

Licha ya AS Vita kuichapa Simba mabao 5-0 katika mchezo wa kwanza  uliochezwa Januari 19, mwaka huu jijini Kinsasha, lakini walishindwa kufurukuta katika mchezo huo wa marudiano.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Ibenge alisema wapinzani wao walikuwa bora sana hasa katika kipindi cha pili cha mchezo huo, hivyo kikosi chake kilishindwa kuhimili vishindo hivyo na kupoteza mchezo huo.

“Simba ni timu nzuri, ilicheza vizuri sana hasa kipindi cha pili, walikuwa na kasi mno, tulijitahidi kupambana nao lakini ilishindikana, tumepoteza mchezo huo na tulistahili kufungwa, wachezaji wangu walionyesha kupoteza umakini na kushindwa kuendana na kasi ya wapinzani wetu.

“Bado nasisitiza kuwa Simba ni timu nzuri na itafanya vizuri sana huko mbeleni, ina wachezaji wazuri na wanajituma zaidi, hivyo wana nafasi nzuri ya kwenda mbali, mimi nawatakia kila la heri kuelekea kwenye michezo hiyo,” alisema Ibenge ambaye pia ni kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,800FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles