23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Kizimbani kwa wizi wa magari manne ya bilioni 1.2/-

AVELINE KITOMARY  Na COSTANCIA MUTAHABA -DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni   Dar es Salaam, imempandisha kizimbani mkazi wa Sinza E,  Venance Mahuma  (45) kwa tuhuma za wizi wa magari manne.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Mfawidhi Godfrey Isaya, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Benson Mwaitenda, alidai mshtakiwa kama mfanyakazi, kati ya tarehe zisizojulikana mwaka 2015 na Februari 2018 katika Mkoa wa Dar es Salaam,   aliiba magari manne.

Magari hayo yote  a ya Zhong Tong ni T 691 DDR, T 562 DDE, T 792 CRB, T 695 CCV yenye thamani ya Sh 1.2 mali ya Salon Zagar ambaye alimpa magari hayo kwa ajili ya biashara.

Mshtakiwa alikana mashitaka na alirudishwa rumande hadi Aprili 29, mwaka huu kesi itakapotajwa tena.

Wakati huo huo, Zena Ibrahim  (30) Mkazi wa Magomeni amepandishwa kizimbani kwa shtaka la kukutwa na noti bandia ya Sh 10,000.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Joyce Mushi, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Abudi Yusuph, alidai   Januari 13, mwaka huu eneo la Bamaga Petrol Station Mwenge Wilaya ya Kinondoni,   alikutwa na noti bandia ya Sh 10,000 yenye namba za usajili 3067553.  

Mshtakiwa alikana mashitaka na alirudishwa rumande hadi Aprili 29 mwaka huu kesi itakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,712FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles