30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kiongozi wa upinzani Algeria akamatwa


ALGIERS, ALGERIA

MFANYABIASHARA na kiongozi wa upinzani nchini Algeria Rachid Nekkaz amekamatwa jana katika hospitali mjini Geneva, Uswisi baada ya kutaka kumfikia rais Abdelaziz Bouteflika anayepokea matibabu katika hospitali hiyo.

Nekkaz anayetaka kuwania urais dhidi ya Bouteflika katika uchaguzi ujao nchini humo amesema alikwenda katika hospitali hiyo kutaka habari zaidi kuhusu Matibabu ya rais huyo mwenye umri wa miaka 82. Aliandaa maandamano madogo nje ya hospitali hiyo kabla ya kutaka kuingia ndani.

Kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi la Polisi nchini humo, Jean-Philippe Brandt ambaye aliviambia vyombo habari kuwa Rachid Nekkaz amekamatwa na jana hiyo alitarajiwa kukabidhiwa kwa mwendesha mashtaka.

Rais Bouteflika, aliyeko madarakani tangu mwaka 1999, hajaonekana hadharani tangu alipougua kiharusi mwaka 2013. Azma yake ya kutaka kuwania muhula mwengine katika uchaguzi wa Algeria unaotarajiwa kufanyika Aprili 18 mwaka huu imesababisha maandamano makubwa nchini humo yanayoongozwa na vijana wanaomtaka Bouteflika kuondoka madarakani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles