27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

’Kepa atabaki kipa namba moja Chelsea’


LONDON, ENGLAND

KOCHA wa Chelsea, Maurizio Sarri, amesisitiza kwamba, mlinda mlango wake, Kepa Arrizabalaga, ataendelea kuwa kipa namba moja japokuwa aliachwa benchi juzi katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tottenham.

Sababu ya mlinda mlango huyo kuachwa benchi ni kutokana na kupishana kauli na kocha huyo katika mchezo wa fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Manchester City mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo Man City iliibuka na ushindi wa mabao 4-3 kwa mikwaju ya penalti baada ya dakika 90 kumalizika bila kufungana.

Katika mchezo huo, kocha huyo alitaka kumfanyia mabadiliko Kepa na nafasi yake ichukuliwe na Willy Caballero, lakini Kepa alionekana kukataa jambo ambalo limemsababishia kukatwa mshahara wa wiki moja wa pauni 195,000.

Kutokana na kitendo hicho, mchezo wa juzi Sarri aliamua kumuweka benchi kipa wake huyo namba moja na nafasi hiyo kuchukuliwa na Caballero.

Hata hivyo, kocha huyo aliwatumia ujumbe wachezaji wote na kuwaambia sababu ya kumwacha benchi Kepa ni kwa kuwa Chelsea ni timu na si mtu mmoja mmoja.

“Bila shaka Kepa ataendelea kuwa kipa namba moja wa Chelsea, lakini mchezo huo dhidi ya Tottenham nilifanya maamuzi sahihi kumuweka benchi Kepa, alifanya kosa kubwa sana katika mchezo uliopita na ndio maana ametakiwa kulipa faini.

“Kutokana na hali hiyo, nikaona bora nimpumzishe lakini kuanzia kesho atakuwa pamoja na sisi, lakini sijui kama mchezaji huyo atakuwa kwenye kikosi cha kwanza katika mchezo unaofuata au atakuwa benchi, ila kwa michezo miwili baadaye ninaamini kwa asilimia kubwa atakuwa kwenye kikosi cha kwanza.

“Hatuna sababu ya kumuulia kiwango chake, lakini ukiwa mdogo lazima ufanya makosa, ila unatakiwa kuwa muelewa kila unapofanya kosa, kwa upande wangu sina tatizo kila kitu kipo sawa,” alisema kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles