25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kabaka awapa mbinu wanawake kusaka kura Pemba

Na KHAMIS SHARIF

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake CCM (UWT), Gaudentia Kabaka, amewataka wanawake wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba wasichoke kuyatangaza mambo yaliyofanywa na Serikali ya Zanzibar.

Pia amewataka watumie lugha fasaha kwa jamii kwani ni mambo ambayo yatasaidia CCM kushinda Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2020 ikiwamo kupata wawakilishi, wabunge na urais.

Hayo aliyasema mwishoni mwa wiki katika ziara yake kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Kabaka alisema sehemu kubwa ya yaliyoahidiwa na Serikali ya Rais Dk. Ali Mohamed Shein yametekelezwa.

Alisema wanawake wa CCM ni tegemeo la chama na pia ndio wapigakura wakubwa, hivyo ni vema watumie lugha fasaha na laini kuwaeleza wasioona utekelezaji wa ilani na huenda ikawa sababu ya kuongeza idadi ya wanachama wapya.

“Sisi wanawake tunakutana na wanawake wenzetu makundi kwa mkundi, sasa tutumieni muda huo kusema kwa vitendo miradi iliyotekelezwa na Serikali ya CCM na hasa huku Pemba, nimeona kuna maendeleo makubwa,” alisema Kabaka.

Asema miradi iliyokwishatekelezwa kama vile barabara, maji safi na salama, afya, elimu na miundombinu mengine iko vizuri kila kijiji, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuyaeleza hayo.

Naye Katibu Mkuu wa UWT, Mwalimu Queen Mlozi, aliwataka wanawake hao kujipanga kimalezi kuhakikisha watoto wao wa kike hawakatishwi masomo kwa sababu ya ndoa.

Alisema mtoto wa kike anatakiwa apitie hatua nne, ikiwemo elimu yake ya msingi na sekondari, chuo kikuu, ndoa na kisha kubeba ujauzito akiwa ndani ya ndoa yake.

“Leo wapo baadhi ya akinamama wamekuwa maadui kwa watoto wao wa kike, kwa kuwakatisha masomo na kuwapa waume, huku wakiwavunjia ndoto zao kama binadamu,” alisema

Kwa upende wake, Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar, Thuwaiba Kisasi, alisema nguvu ya chama ni pamoja na jumuia zake ikiwemo UWT, hivyo kila mmoja ana wajibu wa kusimamia uhai wa chama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles