27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

JPM: Misamaha ya kodi kwa taasisi za dini haijafutwa

Anna Potinus – Dar es salaam

Rais John Magufuli amezitoa wasiwasi taasisi za dini nchini kwa kusema kuwa suala la misamaha ya kodi kwa taasisi hizo halijafutwa kwa sababu zipo sheria zinazosimamia na zinatoa maelekezo ni kwa namna gani wanaweza kupewa misamaha hiyo.

Ametoa kauli hiyo leo wakati akijibu hoja za viongozi mbalimbali wa dini Ikulu jijini Dar es salaam walipokutana kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu nchi ambapo amewataka kutumia misamaha hiyo kama inavyokusudiwa kwani kwa kutokufanya hivyo ni kuwanyima haki wengine ambao hawakupewa misamaha.

“Ninataka niwahakikishie kwamba pale taasisi za dini zinapostahili kupata misamaha ya kodi itaendelea kupewa lakini wito wangu itumike kama ilivyokusudiwa kawasabau zipo taasisi zilizopewa misamaha ya kodi kwaajili ya kujenga miundombinu lakini wanafanyia biashara ushahidi upo kuna sehemu nilienda mimi mwenyewe kununua,” amesema

Aidha amezungumzia suala la wanafunzi wa elimu ya juu wanaokosa mikopo ambapo amesema kuwa wengi wao wanakosea kujaza fomu za kuombea mikopo hiyo na kushidwa kuelewa kuwa bodi ya mikopo haijui matatizo ya.

“Ni kweli wapo watoto wa masikini wengi wanakosa mikopo na hii inatokana na jinsi wanavyojaza fomu zao, ukijaza unaonekana kuanzia vidudu unasoma shule binafsi ya fedha nyingi, msingi hivyo hivyo na sekondari hata kama ulikuwa unasoma kwa msaada inakuwa ngumu kwa bodi ya mikopo kulielewa hilo,” amesema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,573FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles